Monday, November 18, 2019

Boeing Waanza Kuunda NDEGE Zenye Kasi zaidi Mara Tano ya Ndege Zilizopo Sasa

Kampuni ya #Boeing imeanza kushughulikia muundo wa ndege mpya
ya abiria yenye uwezo wa kwenda kasi mara tano ya sauti #Hypersonic.

Tangu kustaafishwa kwa ndege za abiria aina #Concord (supersonic transport) ambazo zilikuwa na uwezo wa kufanya safari zake kwa nusu ya muda unaochukua ndege za sasa, kampuni nyingi zinazo jishughulisha na uundaji wa vyombo vya usafiri wa anga vinajaribu kubuni ndege tofauti tofauti zenye uwezo wa kwenda kasi zaidi ya Concord huku zikitoa udhaifu ulikuwepo wa kelele, uchafuzi mazingira na ulaji mdogo wa mafuta.

Kitendo cha kuunda umbile na injini zitakazoweza kufanya kazi katika kasi inayozidi mara tano ya sauti (zaidi ya 5500km/h) imekuwa ni suala gumu kwani linahitaji fedha nyingi na muda katika uwekezaji na utafiti.

Chombo chochote cha usafiri wa anga kinachotaka kufika mwendokasi huo inahitajika malighafi tofauti katika uundaji wake kama #Titanium ili kukabiliana na joto kali linalosababishwa na msuguano wa chombo husika na hewa.

Kampuni Boeing imekuja na mchoro wa ubunifu wa ngamizi kuonesha ndege hiyo ambayo inategemea kufika mwendokasi zaidi ya 6000km/saa huku ikitumia injini ya #TurboRamjet ambayo ni 'modification' ya ile ambayo awali ilitumika kwenye ndege ya kijasusi aina ya #SR71 "Blackbird" ambayo itakuwa inafanya kazi kama injini ya kawaida ikiwa #Supersonic chini ya mwendokasi wa 4000km/saa na baadae kufanya kazi kama #Ramjet ikifika kasi mara tano ya sauti 'Hypersonic speed' (kuanzia 5000km/saa) kwa kufunga vidirisha upande wa feni za injini hiyo kwakuwa haziwezi tena kufanya kazi katika mwendokasi huo na kuruhusu hewa yenye kasi kuingia moja kwa moja kwenye injini na kuchomwa pasipo kuhitaji mkamizo 'compression' ya injini za kawaida.

Wanasema ndege hiyo itakuwa inaenda usawa wa futi 95,000 kutoka usawa wa bahari na kasi ya 6000km/saa.

Ndege za kisasa kama #Boeing787 #Dreamliner na #Airbus350 #XWB zina uwezo wa kwenda hadi futi 43,000 kutoka usawa wa bahari na kasi ya 930-950km/saa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...