Taasisi ya kizuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imeingilia Kati ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji Cha Kelema Kuu wilayani Chemba baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi iliyofanyika.
Aidha mradi huo wenye thamani ya shilingi 222,978,680 ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.
Hatua hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa moja ya majukumu yake chini ya kifungu cha 7 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.
Hayo yamebainishwa Julai mosi mwaka huu jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya vitendo vya rushwa katika robo ya mwezi April hadi Juni.
Aidha Kibwengo amesema ,katika uchunguzi huo ilibainika kuwa thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa aina ya mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kutokutoa maji.
"Baada ya TAKUKURU kuingilia kati ,mkandarasi wa mradi huo JUIN COMPANY LIMITED ameridhia kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo hulali mosi anaanza kazi ya kubadili mabomba na kuweka yanayostahili,"alisema.
Pamoja na hayo amesema Mkandarasi huyu atarejesha malipo zidifu yaliyolipwa bila kustahili .
"Jumla ya shilingi 67,542,600/= zimeokolewa na tunatarajia wananchi watapata huduma ya maji ,"alisema Kibwengo.
Katika hatua nyingine taasisi hiyo imemkamata Be.Gaston Meltus Francis ambaye ni mkurugenzi wa Global Space East Afrika Limited iliyopewa kazi ya ujenzi wa kituo cha afya Mima wilayani Mpwapwa ambapo kampuni yake ililipwa kiasi cha shilingi 86,405,205 isivyo halali kwa kazi ambazo hazikufanyika katika mradi huo.
Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Dodoma ,uchunguzi huo umeokoa na kurejesha Serikalini jumla ya shilingi 11,877,353 /=zilizolipwa kinyume na taratibu Kama mshahara kwenye akaunti ya benki ya mwalimu aliyefariki.
Aidha kufuatia matukio hayo , TAKUKURU mkoa wa Dodoma inawataka wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaomba wasiwe watazaji bali washiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.
"Tunawataka wanajamii kuwa waangalifu na kamwe wasikubali kurubuniwa na matapeli wanaojifanya maofisa wa TAKUKURU wanaowapigia simu na kuwatisha bali watoe taarifa kupitia namba 113 au kufika katika Ofisi zetu,"alisema Kibwengo.
Source
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
NA REBECA DUWE TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi ...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
