Ngoma za utamaduni wa jamii ya wasukuma huwa ni moja ya kivutio kikubwa wakati wa sherehe za kila mwaka zaJambo Festival wilayani Bariadi. |
Katibu Tawala mkoa wa Simiyu,Jumanne Sagini(kulia) akiwaongoza viongozi kuondoka mara baada ya sherehe zilizoambana na zawadi mbalimbali kwa washiriki kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi. Mwandishi Wetu,Bariadi Watu wenye ulemavu wa miguu mkoani Simiyu wamenufaika kwa kupata msaada wa baiskeli zitakazowawezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila vikwazo baada ya shirika la Wheelchair Foundation la nchini Marekani na Friedkin Conservation Fund (FCF) kutoa baiskeli 48 zenye thamani ya Sh 20 milioni. Mkurugenzi wa taasisi ya Wheelchair Foundation ,Charli Butterfield alimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka baiskeli hizo alisema zitawasaidia watu wenye ulemavu kujishughulisha na shughuli za maendeleo na kuona wapo watu wanaowajali katika hali waliyonayo. Alisema taasisi hiyo imekua ikiwajali watu wenye uhitaji wa baiskeli duniani kote kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita na hapa nchini wameshatoa jumla ya baiskeli 2,240 katika mikoa tofauti na wataendelea kufanya hivyo kadiri wasamaria wema wanavyochangia taasisi yao. Akipokea baiskeli hizo Mkuu wa mkoa huo alisema ni muhimu sana kuwepo na ushirikiano wa kuwafikia wenye ulemavu ambao hawawezi kumudu gharama za kununua baiskeli hizo na kuiomba taasisi hiyo iendelee kusaidia zaidi katika eneo la kuwawezesha watu wenye ulemavu na sekta ya afya na elimu. Aliongeza kuwa wakati wote serikali ya mkoa inatambua ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili za Marekani na Tanzania na mkoa utaendeleza mahusiano hayo kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili katika kuhamasisha maendeleo ya mshikamano. |
Source