Monday, April 29, 2019
Kufanya Mapenzi Mara kwa Mara Kunaboresha Afya yako
Kufanya mapenzi ni mojawapo ya vitu vichache ambavyo watafiti wanasema vinamfanya mtu aburudike huku mwili wake ukifaidika kutokana na tendo hilo.
Utafiti umeonyesha kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kunatibu mafua, kuepusha magonjwa ya moyo, kunazuia kansa na hata kuongeza urefu wa maisha.
Watafiti katika chuo kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza wamegundua kwamba wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara wana uwezekano mdogo sana wa kupata kansa ya kibofu.
Watafiti hao walikanusha madai kwamba kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 20 kwa mwezi kunaongeza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo.
Madaktari wamekubaliana kwamba mapenzi ni kama shughuli zingine za kawaida na ni mazoezi bora kwa afya.
"Kwa kulinganisha na mazoezi, kufanya mapenzi ni sawa na kutembea zaidi ya kilomita moja au kupanda na kushuka ngazi za majengo mawili marefu" alisema Dr Graham Jackson wa hospitali ya St Thomas.
Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Queens University cha Belfast umesema kwamba kufanya mapenzi zaidi ya mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
Tendo la ndoa pia linasaidia kulinda mifupa. Dr Sarah Brewer alisema: "kiwango cha Testosterone kimeonekana kuongezeka wakati tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa".
Utafiti huo ulibainisha kwamba kwa wanaume na wanawake ili waweze kupata faida za tendo la ndoa inawabidi wafanye tendo hilo mara kwa mara.
"Itumie au ipoteze" ndiyo ushauri uliokuwa ukitolewa kwa wazee na wanasayansi toka nchini Finland.
Pamoja na faida za tendo la ndoa ,tendo hilo pia lina hasara zake kama vile kupata magonjwa ya zinaa iwapo kinga haitatumika.
Tangia kugunduliwa kwa viagra miaka 10 iliyopita idadi ya watu wenye umri zaidi ya miaka 45 walioambukizwa magonjwa ya zinaa imeongezeka maradufu.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...