Friday, January 18, 2019
Serikali: Tundu Lissu alishindwa kujibu maswali ya BBC, aliishia kubabaika tu
Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amemjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, akidai kuwa mwakilishi huyo wa wananchi anazungumza uongo kuhusu maendeleo ya Tanzania.
Dk Abbas amesema kwamba licha ya kuulizwa mazuri ya Serikali lakini Lissu alishindwa kujibu na badala yake aliishia kubabaika.
Akihojiwa na kituo cha Utangazaji Uingereza (BBC) jana Januari 16, 2019, Lissu amezungumza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maoni yake kuhusu maendeleo ya nchi, utawala wa katiba na mpango wake wa kugombea urais.
"Unakwenda Ulaya unaponda nchi yako eti haifuati Katiba wakati wewe mwenyewe kuanzia ubunge wako, sifa za ubunge wako na taratibu za uchaguzi wa ubunge wako vyote vipo kwenye Katiba na ndio maana ukawa mbunge," amesema Dk Abbas.
Dk Abbas amedai Lissu hata alipoulizwa mazuri aliyoyaona licha ya changamoto zilizopo, alishindwa kujibu vyema.
"Angalia alivyoshindwa si tu kueleza jema moja la nchi yake baada ya kupewa fursa hiyo, bali kashindwa hata kueleza jema moja alilofanya yeye binafsi jimboni kwake, kaishia kubabaika tu," amedai Dk Abbas.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira tofauti na ile waliyonayo watu wa aina ya Lissu, hivyo itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.
"Sisi tunapigania maendeleo na Watanzania wanaona kazi kubwa inayofanyika kote nchini iwe reli, maji, viwanda, umeme na mambo mengine. Hakuna wa kutuzuia katika kuiletea Tanzania maendeleo. Hakuna," amesisitiza.
Source: Mwananchi
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...