Monday, January 14, 2019
Njia za kuepukana na madeni
Hakuna mtu anayependa kuwa na madeni, lakini mara nyingi watu hujikuta katika madeni makubwa. Kwa kiasi kikubwa watu wengi huingia kwenye madeni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi kuliko kipato.
Madeni siyo kitu kizuri hasa ikiwa hayatalipwa kwa wakati. Swala la kuepuka madeni ni swala linalohitaji maamuzi sahihi ya kifikra pamoja na mikakati stahiki.
Je unapenda kuepuka au kupunguza kiwango chako cha madeni? Karibu nikufahamishe njia za kuepuka madeni.
1. Jiwekee bajeti binafsi
Utawasikia watu wakikosoa bajeti ya serekali lakini hawana bajeti zao binafsi. Bajeti binafsi ni muhimu kwani hukuwezesha kupanga juu ya mapato na matumizi yako.
Ili kuepuka madeni, ni muhimu kuweka bajeti binafsi ambayo itakuongoza juu ya matumizi yako ya pesa ili usije ukatumia kuliko kipato chako.
2. Epuka matumizi yasiyo ya lazima
Kuna matumizi chungu nzima ya pesa, lakini matumizi ya lazima ni machache. Ikiwa kipato chako ni kidogo hakuna haja ya kufanya mambo kama vile kununua simu au nguo za gharama kubwa.
Nimeshuhudia baadhi ya watu wakikopa mikopo kwa ajili ya sherehe na matumizi mengine ya anasa. Mambo kama haya huwaingiza watu wengi kwenye madeni makubwa, hivyo yakupasa kuyaepuka.
3. Epuka kukopa bila mpango
Watu wengi hushindwa kurejesha mikopo kutokana na kukopa bila mpango. Inatakiwa kabla ya kukopa uhakikishe una mpango mzuri unaoonyesha jinsi utakavyotumia na kurejesha mkopo huo.
Kumbuka pesa ya mkopo hasa kutoka kwenye taasisi za kifedha inatakiwa irejeshwe kwa wakati tena kwa riba. Hivyo epuka kutumia pesa za mkopo bila mpango unaoeleweka vyema.
4. Epuka ushawishi wa marafiki kwenye matumizi
Watu wengi hutumbukia kwenye matumizi makubwa au yasiyo na ulazima kutokana na ushawishi wa marafiki kwenye matumizi yao ya pesa.
Hakikisha kila unachokinunua au kutumia pesa yako kina maana kwako na hakitakupotezea pesa zako. Kumbuka mrejeshaji wa mkopo ni wewe na wala siyo rafiki yako
5. Tumia kidogo kuliko unachopata
Mara nyingi matumizi huwa makubwa kuliko kipato; na hii ndiyo sababu kubwa ya watu kukopa pesa. Hakikisha unajitahidi kutumia pesa kidogo kuliko zile unazozipata ili ujiwekee akiba na uweze kukidhi mahitaji yako ya msingi.
6. Weka akiba
Kuna kipindi cha shibe na njaa kwenye uchumi; hivyo unahitaji kujiandaa kwa vipindi vyote. Mara nyingi watu hukopa pindi wawapo na uhitaji.
Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kuwa na pesa hata wakati huna kipato. Kumbuka! Kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi tu.
Kwa hakika nidhamu ya matumizi ya pesa ni jambo muhimu sana katika kuepuka madeni. Naamini pia kama utazingatia hoja jadiliwa hapo juu huku ukihakikisha unakuwa na matumizi mazuri ya pesa, utaweza kupunguza kama siyo kuepuka madeni maishani mwako.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 16, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...