Saturday, October 20, 2018
Watekaji wametelekeza Gari na Silaha 4 Ikiwemo Moja ya Kivita: IGP Sirro
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amezungumzia tukio la kupatikana kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Dewji kutoka kwenye mikono ya watekaji na kusema imebainika nia ya watekaji hao walitaka awapatie pesa.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2018, Sirro amesema; "Nimeambiwa kwamba waliomteka Mohammed Dewji amesema walimwambia walitaka pesa, alipowauliza shilingi ngapi hawakusema, aliwapa simu waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara tungewakamata.
"Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku, MO aliwapa taarifa wazazi wake wakaja kumchukua.
"Watu wetu wako kwenye hizo nchi, tunataka kuwaonyesha ukizoea Tanzania siyo mahali salama, kama walizoea kwenye nchi zao siyo hapa kwetu. Kuacha gari hii na silaha siyo mwisho wa upelelezi. Najua kuna Mtanzania mmoja, tuwapate tuzungumze nao lugha nzuri 'bro',
"Watekaji hao walitaka kuichoma hii gari kupoteza ushahidi, wakajikuta mwisho wa siku wana mashaka na hilo. Inasemekana walikuwa wakizungumza Kiingereza na Kiswahili cha hovyo hovyo, siwezi kusema wametoka nchi gani mpaka pale tutakapowatia mbaroni," alisema Sirro.
Mo Dewji alitekwa alitekwa alhamisi iliyopita, Oktoba 11, 2018 katika gym ya Hotel ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam na kupatikana usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Gymkana baada ya kutelekezwa na watekaji hao.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...