Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii zikidai kuwa kamati kuu ya chama hicho imempitisha kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Monduli Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Kamati Kuu ya (CHADEMA), imekutana katika kikao chake maalum jana Jumatano Agosti 15, 2018 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu chama hicho na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na tovuti ya www.eatv.tv Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa amesema kuwa taarifa za kuteuliwa Lowassa hazina ukweli wowote kwani kufanya hivyo ni kumshusha hadhi Waziri Mkuu huyo mstaafu na kudai kuwa hadhi yake kwa sasa ni nafasi ya urais.
"Hayo sio mapendekezo ya kamati kama wanavyosema na hizo ni taarifa za uzushi na zinafanywa na wapinzani wetu kutaka kutuchafua, hakuna mgombea aliyepitishwa na mapendekezo yote yaliyotolewa ni ya awali," amesema Golugwa.
Akizungumzia uamuzi wa Fred Lowassa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge jimbo la Monduli, Golugwa amesema baada ya kushauriana, vikao vya uteuzi vilikubali kuondoa jina lake.
Fred ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, alichukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo wiki iliyopita lakini jana aliomba kujiondoa kwakile alichodai kuwa bado muda wake muafaka licha ya kuonekana kuungwa mkono na wanachama wengi awali.
Baada ya kujiondoa, Chadema kimempitisha diwani wa kata ya Lepurko, Yonas Masiaya Laizer kuwania ubunge wa jimbo hilo, kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga, kuachana na Chadema na kuachia ubunge na kuhamia CCM, ambapo Kalanga ameshateuliwa na CCM kugombea tena jimbo hilo.
Source
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
