Thursday, October 3, 2019

NCHIMBI,MOLINGA BALAA SANA....WAPIGA SHOO YA KIBABE YANGA IKITOKA SARE NA POLISI

Na  Olipa Assa - Mwanaspoti
 Mshambuliaji, Ditram Nchimbi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu kufunga hat trick msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania.

Nchimbi amefunga mabao hayo Leo Alhamisi wakati timu yake ya Polisi Tanzania ikilizimisha sare 3-3 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Nchimbi alifunga mabao yake katika dakika ya 34, 55 na 58 na kuifanya Yanga kuwa nyuma kwa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Hata hivyo furaha hiyo ya Polisi Tanzania ilidumu kwa muda mfupi baada ya mshambuliaji David Molinga akifunga mabao mawili katika dakika ya 65 na 68 kuisawazishia Yanga.

Hayo ni mabao ya kwanza kwa Molinga kufunga katika Ligi Kuu Bara, moja akifunga goli la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliipigwa na Ngassa kabla ya kupachika la pili kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe za mashabiki wa Yanga.


Molinga hakuanza vizuri dakika 45 za mwanzo alirejea kwa kishindo na kuwapa nguvu mashabiki wa Yanga waliokuwa nyuma kwa mabao 3-1 hadi dakika ya 64.

Lissu asaini mkataba na kampuni ya kimataifa kumsimamia kisheria


Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesaini mkataba maalum na kampuni ya kimataifa ya kisheria ya Amsterdam and Partners LLP akiwapa jukumu la kusimamia haki zake za kikatiba na za kimataifa.

Kampuni hiyo imetoa taarifa yake jana, Oktoba 2, 2019 ikieleza kuwa imefurahi kufanya kazi na Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

"Tunajivunia kufanya kazi na Tundu Lissu katika kuongeza uelewa kwenye hali yake na kampeni dhidi ya uvunjifu wa sheria na haki za kisiasa," imeeleza kampuni hiyo.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alipoenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa kwa risasi, alitangaza kuahirisha kurejea nchini Septemba 7 mwaka huu kama alivyoahidi ili akutane kwa mara nyingine na madaktari wake.

Mwanasiasa huyo alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa maeneo ya nyumbani kwake, Area D jijini Dodoma.

Alipatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kisha akapelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi, kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji alikoendelea kupatiwa matibabu hadi leo.

Kampuni ya Amsterdam and Partners LLP yenye makazi yake jijini London nchini Uingereza, kazi yake kubwa ni kuwashauri wateja hususan kwenye changamoto kubwa za kisheria.

Wanawake Waonywa Kuhusu Kutumia Mvuke wa Moto Sehemu za Siri


Madaktari wa magonjwa ya wanawake wameonya kuhusu hatari inayotokana na kutumia mvuke wa moto kwenye sehemu za siri, baada ya kutokea kuwa mwanamke mmoja alijiunguza sehemu zake za siri alipo kuwa akitumia mvuke wa maji kufusha au kufukiza sehemu za siri.

Waswahili husema urembo unauma. Je ni maumivu kiasi gani unayoweza vumilia ili kupata urembo au kupendeza?
4h

MGANGA WA KIENYEJI ADAIWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 MAMA AKINUNUA WEMBE


Mganga wa kienyeji mkazi wa Ujiji, Venas Edward (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Mkoa wa Kigoma kwa madai ya kumbaka mtoto msichana mwenye umri wa miaka minane.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana.

Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Raymond Kimbe, ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo ya awali Wakili wa Serikali Kimbe, alidai kuwa Aprili 23, mwaka huu majira ya asubuhi eneo la Kasoko-Ujiji, mshtakiwa huyo alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka minane na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Kimbe alidai siku ya tukio mtoto huyo alichukuliwa na mama yake mzazi (jina linahifadhiwa) na kwenda naye kwa mshtakiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu.

Alidai baada ya kufika kwa mganga huyo mama wa mtoto aliambiwa aende kununua kiwembe dukani na kumuacha mtoto na mganga huyo, ambaye anadaiwa alitumia nafasi hiyo kumbaka mtoto huyo.

Kufuatia tukio hilo ilidaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na askari polisi na baada ya mahojiano alipelekwa mahakamani.

Wakili huyo alidai upande wa mashtaka unatarajia kupeleka mashahidi watano pamoja na kielelezo kimoja cha PF 3 na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi.

Hakimu Mwakitalu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9 kwa kusikilizwa.

Source

Friday, September 27, 2019

Bashe Asema kuna upotevu wa zaidi ya Bilioni 120 kwenye vyama vya ushirika



Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.

"Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote," amesema.

"Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua," amesema Bashe.

Aidha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi  kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.

DC MWAIMU AWATANGAZIA KIAMA WANAOJUMU MIRADI YA MAENDELEO KYERWA

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwaimu

Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Mhe. Rashid Mwaimu 
amesema atapambana vikali usiku na mchana ili kuhakikisha anakomesha watu wanaotaka kuhujumu miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi itolewayo na serikali akibainisha kuwa yupo tayari kukesha katika maeneo yote ya miradi ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya hiyo Rashid Mwaimu ametoa kauli hiyo Septemba 27.2019 ofisini kwake wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo wilayani hapo.

Mhe.Rashid amesema atahakikisha analinda na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoletwa na serikali wilayani humo huku akiahidi kuwashughulikilia wale wanaokutaka kufanya vitendo vya kuihujumu serikali.

Amesema kutokana na jitihada, nguvu na busara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika utekelezaji wa miradi ya ki maendeleo yeye kama mkuu wa wilaya hatomfumbia macho mtu yeyote anayepanga kuhujumu miradi hiyo.

"Nawaahidi miradi yote inayoletwa na serikali kwa ajili ya wilaya ya Kyerwa nitaisimamia na kuilinda kwa nguvu zote, nitahakikisha adui yeyote haisogelei miradi hiyo ,miradi ni mali ya wananchi ole wenu mliozoea kuitafuna muda umekwisha, nitacheza na nyie usiku kucha", alisema Mwaimu.

Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahimiza kutomchagua kiongozi mbishi, badala yake wachague kiongozi ambaye ni mzalendo na muadilifu atakayewaletea maendeleo.

Katika suala la ulinzi na usalama, amesema katika wilaya yake ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo amewataka wananchi kuripoti katika vyombo husika mara moja vinapojitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa baadhi ya watu wasiowaadilifu hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

KITABU CHA KUSAIDIA WANAWAKE WANAOWANIA NAFASI ZA UONGOZI CHAZINDULIWA KWENYE TAMASHA LA JINSIA 2019


Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukifanyika leo  Alhamis Septemba 26,2019 kwenye usiku wa Mwanamke wa Kiafrika wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. Lengo la kitabu hicho ni kutoa taarifa muhimu kuhusu mashirika yanayosaidia jitihada za wanawake kuwania nafasi za uongozi kwa ngazi zote na kwa wanawake wa vyama vyote vya siasa. Kitabu hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Women Fund Tanzania kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya na Seidel Foundation. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.

Wednesday, September 25, 2019

VIDEO: Kocha Simba atamba kuishangaza Kagera Sugar


Kocha mkuu wa timu ya Simba, Patric Ausemsi ametamba kuondoka na pointi tatu muhimu katika uwanja wa Kaitaba katika mchezo ligi kuu ya Tanzania bara dhidi Kagera Sugar huku wachezaji wake wanne tegemeo wakiukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE


Source

ASKOFU MKUU YUDA THADEUS RUWA'ICHI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI MOI LEO.....AMSHUKURU RAIS MAGUFULI NA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiongea kwa furaha na wanahabari mara baada ya kuruhusiwa kuondoka Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. 


Wengine ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia). 

Mhashama Askofu Mkuu Ruwa'ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu 

Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam  Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MOI) pamoja na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa  wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface (wa pili kushoto)  na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba (kulia) baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano Septemmba 25, 2019.


Mhashama Askofu Mkuu Ruwa'ichi, ambaye alifikishwa hapo MOI  akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo, amemshukuru Mungu kwa yote na pia amemshukuru  Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa msaada wa haraka wa ndege ya Rais kumsafirisha hadi Dar es salaam alikopatiwa matibabu.


Pia amewashukuru Madaktari wa KCMC kwa matibabu ya awali na wa MOI kwa kuokoa maisha yake kwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Vile vile amewashukuru waumini na Watanzania wote kwa ujumla kwa kumuombea.

PICHA NA ISSA MICHUZI



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...