Thursday, October 3, 2019
Lissu asaini mkataba na kampuni ya kimataifa kumsimamia kisheria
Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesaini mkataba maalum na kampuni ya kimataifa ya kisheria ya Amsterdam and Partners LLP akiwapa jukumu la kusimamia haki zake za kikatiba na za kimataifa.
Kampuni hiyo imetoa taarifa yake jana, Oktoba 2, 2019 ikieleza kuwa imefurahi kufanya kazi na Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
"Tunajivunia kufanya kazi na Tundu Lissu katika kuongeza uelewa kwenye hali yake na kampeni dhidi ya uvunjifu wa sheria na haki za kisiasa," imeeleza kampuni hiyo.
Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alipoenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa kwa risasi, alitangaza kuahirisha kurejea nchini Septemba 7 mwaka huu kama alivyoahidi ili akutane kwa mara nyingine na madaktari wake.
Mwanasiasa huyo alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa maeneo ya nyumbani kwake, Area D jijini Dodoma.
Alipatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kisha akapelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi, kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji alikoendelea kupatiwa matibabu hadi leo.
Kampuni ya Amsterdam and Partners LLP yenye makazi yake jijini London nchini Uingereza, kazi yake kubwa ni kuwashauri wateja hususan kwenye changamoto kubwa za kisheria.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Kulia ni Mkurugenzi wa Stedom House of Beauty Bi. Stella Mhondo akigonga Cheers na wadau wa masuala ya Urembo na Vipodozi waliohudhuria uzin...
-
NA REBECA DUWE TANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi ...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
