Friday, November 2, 2018

Wema Sepetu Aburuzwa Tena Mahakamani

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameonekana kushindwa kukaa mbali na mahakama kwani miezi michache baada ya kesi yake ya madawa ya kulevya kuisha  mrembo huyo amerudi kizimbani kwa kesi ya kusambaza picha chafu kwenye mitandao ya kijamii. Siku ya jana Novemba 01, 2018  Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya kuburuzwa mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya Kusambaza picha za faragha mtandaoni. Wema Sepetu alipata dhamana mahakamani hapo baada ya kukidhi vigezo, ambapo moja ya sharti lilikuwa ni kupata mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Milioni 10. Sharti lingine alilopewa kwenye dhamana hiyo, ni kutoposti picha au video zenye maudhui ya ngono kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo amekana shtaka hiloo, na kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tena Novemba 20 mwaka huu.

The post Wema Sepetu Aburuzwa Tena Mahakamani appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

ZITTO KABWE ASOMEWA MASHTAKA YA UCHOCHEZI

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya Jeshi la Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hata hivyo ,Zitto amekana kwa kusema sio kweli na muda huu yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri uamuzi wa dhamana.

Zitto Kabwe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo Novemba 2,2018 baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Oktoba 31, 2018.

Zitto anatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Zitto, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini, mara baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye Kituo cha polisi cha Oysterbay, kabla ya kuhamishiwa polisi kati na baadaye kulazwa kwenye kituo cha polisi Mburahati.

Kabla ya kukamatwa na Polisi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno, alimtaka Zitto kuwasilisha alichokiita, "vielelezo vya madai yake," kuwa watu zaidi ya 100 wameuwa katika eneo la Uvinza.

Magufuli :Tanzania is on the right path

President John Magufuli yesterday stole the show at a symposium that deliberated on achievements and challenges during the three years of his presidency.
Source

Thursday, November 1, 2018

DC Katambi atinga Stesheni ya Dodoma, Atishia Kuwatumbua


MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi ametishia kuwatumbua watumishi wa Stesheni ya Treni endapo hawatotekeleza maagizo maagizo yake.

DC Katambi ametoa kauli hiyo leo alipofika katika stesheni hiyo baada ya kupigiwa simu na abiria waliokua wamekwama tangu jana kufuatia treni mbili kukutana.

Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kuzungumza na abiria hao ambao aliwaomba kutulia huku akiuagiza uongozi wa Reli kuwatafutia usafiri mwingine wa kuwapeleka jijini Dar es Salaam pia alikagua mazingira ya stesheni hiyo kutokana na kulalamikiwa na wasafiri hao.

" Nimepita kukagua mazingira ya stesheni yetu, nimekutana na mambo mengi ya hovyo ambayo yanaweza kutatulika ili kuondoa kero za abiria wetu ambao kimsingi ni Watanzania wenzetu ambao wanalipa kodi ya Nchi yao kwa kulipa nauli.

" Stesheni kubwa kama hii haina vyoo vya kutosha na vilivyopo vimeziba kutokana na wingi wa vinyesi, maji hakuna pia kwa sababu stesheni inadaiwa na nimewaagiza kulipa deni wanalodaiwa. Na wasipotekeleza basi wajue nitawatumbua," amesema DC Katambi.

Charles James.

LOWASSA AZUIWA POLISI


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amezuiwa kumuona kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe anayeshikiliwa na polisi tangu jana Oktoba 31, 2018.


Msaidizi wa waziri mkuu huyo wa zamani, Aboubakary Liongo amesema kuwa leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 saa 9 Alasiri Lowassa alikwenda kumuona Zitto kutaka kujua hatima yake, kwani wako pamoja naye kuhakikisha haki inatendeka, lakini akaelezwa kuwa muda wa kumuona umeshapita.

Baada ya kufika kituoni hapo, msaidizi wa Lowassa alikwenda kuomba kibali cha kumuona Zitto lakini alielezwa kuwa muda umekwisha, ambapo Lowassa amenukuliwa akisema, "Huyu ni kiongozi mwenzetu huku upinzani lazima tushikamane kukabiliana na lolote lililo mbele yetu, tunahitaji kuwa kitu kimoja kuliko wakati mwingine wowote".

Zitto yupo kituo cha polisi Mburahati ambako alipelekwa jana baada ya kutolewa kituo cha kati Polisi makau makuu akitokea kituo cha Osterbay alikohojiwa kwa zaidi ya saa 3 baada ya kukamatwa akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam.

Chanzo- EATV

Pressure builds on ILO to cut tobacco ties

Geneva, Switzerland /AFP /.More than 100 groups urged the International Labour Organization to stop taking money from tobacco companies as the UN body prepared Wednesday to once again debate the controversial issue.
Source

Rais Magufuli: Sina mpango wa kutoa pesa kwa ajili ya katiba mpya

Rais Magufuli: Sina mpango wa kutoa pesa kwa ajili ya katiba mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewataka watu wanaotegemea atoe pesa kwa ajili ya kukaa vikao kujadili masuala ya kubadilisha katiba ya nchi waache kwa sababu hana mpango wala hategemei kutoa pesa kwa ajili hiyo.

Amesema kwa wale wenye fedha wanaotaka kusaidia mpango huo wampatie ili akamalizie mradi wa kujenga reli mpya ya kisasa ya Stiegler's Gorge.

Ameyasema hayo leo Alhamis Novemba Mosi  alipokuwa akizungumza na washiriki wa kongamano la kuijadili hali ya siasa na uchumi wa nchi lililojumuisha maprofesa na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali za serikali na Jeshi, lililofanyika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais Magufuli amesema amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kubadilisha Katiba mpya wasidhani hajui umuhimu wake ila kwa sasa hana pesa za kufanya hivyo.

"Sitegemei kutoa hela kwa ajili ya watu kwenda kujadili masuala ya kubadili katiba kama watu wana hizo hela watupe tukamalizie mradi wa Stieglers George," amesema.

Rais Magufuli amesema hali ya uchumi ya nchi kwa sasa inakuwa kwa asilimia saba na  na Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na mambo yakienda kama yalivyo pangwa itaendeleakukuwa na atasimamia hili ili ikue zaidi ya hapa.

"Nchi yetu ilifika katika hatua  kubwa sana ya rushwa na ndiyo maana  niliamua kujipa kazi kubwa ya kutumbua majipu kwa sababu nilitaka kufikisha nchi sehemu nzuri pamoja na changamoto zake niliapa lazima tutafika tu.

"Katika mambo makubwa ya msingi ni lazima tuyasimamie kwa pamoja kama watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa na vyama na tusikubali kutumiwa,"amesisistiza Magufuli.

Steve :-Adhabu ya Kufungiwa kwa Wema ni Ndogo Sana.

Ikiwa ni siku chache tangu mwanadada Wema Sepetu aanze kupokea adhabu zak kutokana na kosa lake la kuvujisha video katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanaume faragha, watu mbalimbali wamekuwa wakiongea misimamo yao kuhusu swla hilo huku wengine wakionekana kumtetea na kuomba mamlaka husika kumuangalia kwa jicho la pili na kumuonea huruma kumsamahe lakini kwa upande wa steve nyerere yeye anasema kuwa wema amekosea na anahijati adhabu. Steve anasema kuwa pamoja na kwamba woa ni marafiki wa watu wa karibu kwa muda mrefu lakini anaona kabisa kuwa kwa swala hili alilofanya wema amekosea na kuangusha taifa hivyo hawezi kuungana nae mkono hata mara moja. Stev anasema kuwa Wema sepetu ni msanii mkubwa ambae amekuwa akiitangaza tanzania nje ya nchi hivyo kwa hilo alilofanya limeonekana kote na waa sio tanzania tu hivyo wala hapaswi kuhurumiwa hata kidogo. Lakini pia Steve anasema kuwa kwa adhabu ambayo Wema amepewa na bodi ya filamu nchini haoni kama ina ukubwa wowote kulingana na kosa alilofanya. kwanza niseme ukweli kuwa kwa  adhabu anazopewa wema sio kwamba anaonewa lakini ni kwa sababu wnataka kuwanusuru watoto wetu jamani,naona hii adhabu ya kufungiwa ni ndogo alitakiwa kupewa adhabu kubwa zaidi, na hapo bado TCRA nao watakuja na adhabu yao.

The post Steve :-Adhabu ya Kufungiwa kwa Wema ni Ndogo Sana. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Idara ya Uhamiaji Nchini Yakamata Wahamaji Haramu 10,.396


Wahamiaji hao wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu, kati ya hao 5,453 waliondoshwa nchini

Aidha, wengine 2,181 wamefikishwa Mahakamani kwa makosa ya uhamiaji na waliofungwa kwenye magereza mbalimbali ni Wahamiaji 240
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...