Thursday, November 1, 2018
DC Katambi atinga Stesheni ya Dodoma, Atishia Kuwatumbua
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi ametishia kuwatumbua watumishi wa Stesheni ya Treni endapo hawatotekeleza maagizo maagizo yake.
DC Katambi ametoa kauli hiyo leo alipofika katika stesheni hiyo baada ya kupigiwa simu na abiria waliokua wamekwama tangu jana kufuatia treni mbili kukutana.
Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kuzungumza na abiria hao ambao aliwaomba kutulia huku akiuagiza uongozi wa Reli kuwatafutia usafiri mwingine wa kuwapeleka jijini Dar es Salaam pia alikagua mazingira ya stesheni hiyo kutokana na kulalamikiwa na wasafiri hao.
" Nimepita kukagua mazingira ya stesheni yetu, nimekutana na mambo mengi ya hovyo ambayo yanaweza kutatulika ili kuondoa kero za abiria wetu ambao kimsingi ni Watanzania wenzetu ambao wanalipa kodi ya Nchi yao kwa kulipa nauli.
" Stesheni kubwa kama hii haina vyoo vya kutosha na vilivyopo vimeziba kutokana na wingi wa vinyesi, maji hakuna pia kwa sababu stesheni inadaiwa na nimewaagiza kulipa deni wanalodaiwa. Na wasipotekeleza basi wajue nitawatumbua," amesema DC Katambi.
Charles James.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...