Friday, November 2, 2018

Wema Sepetu Aburuzwa Tena Mahakamani

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameonekana kushindwa kukaa mbali na mahakama kwani miezi michache baada ya kesi yake ya madawa ya kulevya kuisha  mrembo huyo amerudi kizimbani kwa kesi ya kusambaza picha chafu kwenye mitandao ya kijamii. Siku ya jana Novemba 01, 2018  Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya kuburuzwa mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya Kusambaza picha za faragha mtandaoni. Wema Sepetu alipata dhamana mahakamani hapo baada ya kukidhi vigezo, ambapo moja ya sharti lilikuwa ni kupata mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Milioni 10. Sharti lingine alilopewa kwenye dhamana hiyo, ni kutoposti picha au video zenye maudhui ya ngono kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo amekana shtaka hiloo, na kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tena Novemba 20 mwaka huu.

The post Wema Sepetu Aburuzwa Tena Mahakamani appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...