Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewataka watu wanaotegemea atoe pesa kwa ajili ya kukaa vikao kujadili masuala ya kubadilisha katiba ya nchi waache kwa sababu hana mpango wala hategemei kutoa pesa kwa ajili hiyo.
Amesema kwa wale wenye fedha wanaotaka kusaidia mpango huo wampatie ili akamalizie mradi wa kujenga reli mpya ya kisasa ya Stiegler's Gorge.
Ameyasema hayo leo Alhamis Novemba Mosi alipokuwa akizungumza na washiriki wa kongamano la kuijadili hali ya siasa na uchumi wa nchi lililojumuisha maprofesa na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali za serikali na Jeshi, lililofanyika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Rais Magufuli amesema amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kubadilisha Katiba mpya wasidhani hajui umuhimu wake ila kwa sasa hana pesa za kufanya hivyo.
"Sitegemei kutoa hela kwa ajili ya watu kwenda kujadili masuala ya kubadili katiba kama watu wana hizo hela watupe tukamalizie mradi wa Stieglers George," amesema.
Rais Magufuli amesema hali ya uchumi ya nchi kwa sasa inakuwa kwa asilimia saba na na Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na mambo yakienda kama yalivyo pangwa itaendeleakukuwa na atasimamia hili ili ikue zaidi ya hapa.
"Nchi yetu ilifika katika hatua kubwa sana ya rushwa na ndiyo maana niliamua kujipa kazi kubwa ya kutumbua majipu kwa sababu nilitaka kufikisha nchi sehemu nzuri pamoja na changamoto zake niliapa lazima tutafika tu.
"Katika mambo makubwa ya msingi ni lazima tuyasimamie kwa pamoja kama watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa na vyama na tusikubali kutumiwa,"amesisistiza Magufuli.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...