Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, amesisitiza dhamira ya kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo, wakiwemo Amref Health Africa Tanzania, katika kuimarisha huduma za afya na maendeleo endelevu ya jamii.
Akizungumza alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, Oktoba 19, 2026, Balozi Brennan amesema mkakati mpya wa Ireland nchini utaunga mkono vipaumbele vya maendeleo vya Tanzania, ukiweka mkazo kwa wanawake, wasichana na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ameeleza kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanga unachangiwa na sekta mbalimbali, ikiwemo afya na kilimo.
Ireland Tanzania inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo kuimarisha huduma za afya na kuleta mabadiliko chanya na endelevu katika jamii.




