
13 Oktoba 2025
📍Kata ya Bwilingu – Mdaula, Msolwa na Chalinze Mzee
🌍 Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani
🆕Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ameendelea na ziara zake za kampeni kwa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa kata ya Bwilingu, akitembelea maeneo ya Mdaula, Msolwa na Chalinze Mzee. Ziara hii ni sehemu ya jitihada za kuomba ridhaa ya wananchi wa Chalinze ili CCM iendelee kuongoza serikali kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Katika mikutano hiyo, Mheshimiwa Kikwete amewapongeza wananchi kwa moyo wa uzalendo na mshikamano waliouonyesha kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi chote, na amewaomba kuendelea kuamini katika chama chenye historia ya kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wakazi wa maeneo hayo, amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni matunda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Katika miaka minne pekee, Rais Samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi shupavu na jemedari wa maendeleo ya wananchi. Ametekeleza ilani ya uchaguzi kwa umahiri, uaminifu na weledi mkubwa katika sekta zote ikijumuisha afya, elimu, miundombinu, maji na huduma za kijamii," alisema Mheshimiwa Ridhiwani.
Amewahakikishia wananchi kuwa CCM itaendelea kuwa jibu sahihi kwa changamoto zao, akisisitiza kuwa chama hicho kina watu, sera na uzoefu wa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.
Pia amewakumbusha wananchi kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 ni siku muhimu ya kufanya maamuzi ya kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana, kwa kumpigia kura mgombea wa CCM wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani, ili kuhakikisha ushindi mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#ChalinzeYaMaendeleo
#IlaniImetekelezwa
#RidhiwaniNiChaguoSahihi
#SamiaNiTumainiJipya
#CCMKweliInatekeleza
#MaendeleoKwaVitendo
#ChalinzeMpya2025



