Saturday, March 22, 2025
Manara: Huu ni Mwaka wa Uchaguzi Msigombanishe Serikali na Wananchi Kwa Maswala ya Simba na Yanga
KLABU YA COASTAL UNION YAPOKEA BASI JIPYA KUTOKA BENKI YA NBC
Maajabu! MTI ULIOANGUSHWA NA UPEPO, UKAKATWA ,WASIMAMA TENA GEITA

Mti huo, unaomilikiwa na Kanisa la Golan Gospel Center lililopo mtaani hapo, umeibua mijadala kuhusu uwezekano wa tukio hilo kuwa la miujiza.
Baadhi ya viongozi wa kanisa na wananchi wameeleza kushangazwa na hali hiyo.
Katibu wa Kanisa la GGC, Yohana Mathias, amesema tukio hilo limewashangaza waumini wa kanisa na wakazi wa Mpomvu, huku wengine wakilihusisha na nguvu za kiimani.
Mkazi wa Mpomvu, Emmanuel Lameck, amesema hajawahi kushuhudia jambo kama hilo maishani mwake na kwamba bado linafikirisha.
Naye Stella Saimon, mkazi wa Mpomvu, amekiri kuwa tukio hilo limeleta mshtuko kwa wengi, huku wengine wakitafsiri kuwa ni tukio la kiimani au la kishirikina.
Mchungaji wa Kanisa la Golan Gospel Center, Jefta Lameck, amesema mti huo ulikuwa wa muda mrefu, na baada ya kuangushwa na upepo, waliamua kuukata kwa kuwa ulikuwa umezuia njia. Hata hivyo, walipofika asubuhi iliyofuata, walikuta mti huo umesimama tena hali iliyozua mshangao mkubwa.
Amesema tukio hilo lisihusishwe na imani za kishirikina na amewataka wananchi kuwa watulivu huku wakilitafakari kwa mtazamo wa kawaida wa kimaumbile badala ya kuingiza hofu au imani potofu.
Chanzo - Maduka Online Blog
Wamarekani Hawautaki Ushirikiano wa TRUMP na Elon Mask, Washambulia Magari ya Tesla
Mashambulizi dhidi ya vituo vya Tesla yameongezeka baada ya #ElonMusk kushirikiana na utawala wa #Trump kwenye Idara ya Ufanisi wa Serikali (#DOGE), ambayo imepunguza matumizi makubwa ya serikali.
Miji kama Portland na Seattle imeathirika zaidi, huku magari ya Tesla, vituo vya kuchaji, na stoo za magari vikilengwa. Kwenye shambulio moja #LasVegas, magari kadhaa yaliwashwa moto na neno "#resist" likaandikwa kwenye jengo.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Pam Bondi, alisema watu watatu waliokamatwa kwa mashambulizi hayo wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 kwa ugaidi wa ndani.
Trump alitumia #TruthSocial kutangaza kuwa wahusika wanapaswa kufungwa kwa miaka 20 na kupendekeza wafungwe katika magereza ya #ElSalvador, akiyataja mashambulizi hayo kama ugaidi wa ndani. Alisisitiza kuwa Tesla ni "kampuni kubwa ya Marekani" na hata kununua gari lake la #Tesla kuonyesha uungaji mkono.
Friday, March 21, 2025
DR. MPANGO AWAFARIJI WAFIWA MSIBA WA HAWASSI
Ripoti Ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii Katika Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto Yaonesha Changamoto Kadhaa Babati
Na John Walter -Babati
Marafiki wa Elimu wilaya ya Babati wamewasilisha ripoti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto.
Ripoti hiyo, iliyowasilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Benjamin Richard, inaonesha changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto katika malezi, usalama, na mazingira ya kujifunzia.
Utafiti huu ulifanyika katika kata nne za Babati ,Bagara, Maisaka na Nangara kwenye shule za Msingi 16, ambapo wadau mbalimbali walihojiwa, wakiwemo watendaji wa kata, wamiliki wa vituo vya kulelea watoto (day care), walimu, wawakilishi wa asasi za kiraia, viongozi wa serikali za mitaa na vijiji, pamoja na wazazi wenye watoto katika shule za awali.
Matokeo Muhimu ya Ripoti
Usalama wa Watoto Shuleni
- Kati ya shule 16 zilizotembelewa, hakuna hata moja yenye uzio, hali inayohatarisha usalama wa watoto.
- Shule nyingi zipo karibu na barabara, hivyo kuongeza hatari kwa watoto.
Adhabu kwa Watoto
- Asilimia 11.2 ya waliohojiwa walithibitisha kuwepo kwa adhabu za kuumiza katika baadhi ya shule.
- Hata hivyo, asilimia 60 ya wazazi na walimu walikiri kuwa shule ni salama na wanatambua umuhimu wa ulinzi na usalama wa watoto.
Afya na Mazingira ya Shule
- Asilimia 68 ya vyoo vya shule si salama kwa watoto, hali inayohatarisha afya zao.
- Ni shule tano pekee ndizo zenye vyoo maalum kwa wanafunzi wa awali.
Malezi na Muda wa Wazazi na Watoto
- Asilimia 93.7 ya watu 168 waliohojiwa walikiri kuwa wazazi wengi hawana muda wa kukaa au kucheza na watoto wao.
- Wazazi wengi wamekuwa wakiacha majukumu yao kwa wafanyakazi wa ndani, ambao mara nyingi huonekana kama mama na baba wa watoto hao.
Hatua Zinazochukuliwa
Baada ya uwasilishaji wa ripoti hii, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Marafiki wa Elimu Babati, Gaudencia Igoshalimo, amesema kuwa watarejea kwa wananchi kwa ajili ya kuhamasisha marekebisho ya changamoto zilizobainika.
Marafiki wa Elimu Babati, chini ya mwavuli wa HakiElimu, wanatekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha mazingira ya watoto, ikiwa ni pamoja na:
- Ujenzi wa vyoo katika shule tano ili kuboresha usafi na usalama wa wanafunzi.
- Ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Nakwa, ambapo wazazi watachangia ujenzi wa msingi na HakiElimu itakamilisha mradi huo.
Wito kwa Wazazi
Wazazi wametakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto wao badala ya kuwaachia malezi kwa wafanyakazi wa ndani pekee.
"Wazazi waache tabia ya kuwa bize na maisha huku wakitelekeza watoto wao, ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto anapata malezi bora na muda wa kufundwa katika misingi sahihi ya maisha," ilisisitizwa katika ripoti hiyo.
Kwa hatua hii, Marafiki wa Elimu Babati wanaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika mazingira salama, yenye afya, na yanayochochea maendeleo yao ya elimu na maisha kwa ujumla.
Picha mbalimbali wakati wa Uwasilishaji ripoti.
Bosi Hakujua Kama Nimemfunga Mke wangu
Jina langu Abdallah, unajua wahenga hawakukosea waliposema ukistaajabu ya musa utayaoana ya firauni, huu ni msemo ambao hadi sasa unaishi katika maisha ya watu na jamii kwa ujumla kutokana na matukio na visa mbalimbali vinavyowakumba.
Singependa kutaja jina langu kutokana sababu za kiusalama ila naishi nchini Kenya, nimeamua kuandika ujumbe huu baada ya Bosi wangu kuleta mambo ya ajabu sana, nayo ni kung'ang'ania kuzaa mtoto na mke wangu wa ndoa.
Hata hivyo, mke wangu hakujua kama nimemfunga, wala Bosi wangu hakujua hilo, hivyo nilipokuwa napata safari za kikazi nilikuwa na amani tele na furaha zaidi hasa kutokana na kuongezeka kwa fedha ambayo nilikuwa napatiwa kama posho ya kujikimu na safari.
Baada ya muda wa miezi kadhaa mke wangu aliniita chumbani na kuniambia Bosi wangu alikuwa akimtongoza na kumwambia anataka kuzaa naye kutokana anaona watoto wetu ni wazuri sana na wanavutia.
Mke wangu aliniambia kwa muda mrefu alifanya jambo hilo kuwa siri lakini anaona kadiri anavyofanya siri moyo wake unakosa amani kabisa kutokana na jinsi anavyosumbuliwa.
Alilia sana na kuniomba msamaha kwa kutunza siri hiyo ya ajabu ambayo ingeweza kumfanya akazaa nje ya ndoa yetu ambayo imedumu kwa miaka mingi sasa, huku ikiwa na amani na upendo.
Hadi kufika hapo nikajua kabisa dawa ya Kiwanga Doctors kweli inafanya kazi yake ipasavyo, kilichokuja kunishangaza ni yule Bosi wangu alikuja kufukuzwa kazi katika mazingira ambayo sikuwahi kuyaelewa hadi sasa na hapo ndoa yangu ikazidi kuwa na usalama zaidi.
Unajua tulifikaje hapo?. kwa uwezo wa Kiwanga Doctors kutoka Migori, Kenya ndipo nilipobaini mbinu hiyo chafu ya Bosi wangu, nakumbuka nafiki yangu mmoja alinipa namba ya mtaalamu huyo na kuniambia anaweza kumfunga mke wangu asiweze kutoka nje ya ndoa.
Nilifika ofisini kwake na alinipatia dawa na kuanza kuzitumia, niliendelea na shughuli zangu, wakati huo Bosi wangu alikuwa kila mara ananipa safari nyingi za kikazi ili apate muda wa kuendelea kumshawishi mke wangu bila kujua tayari nilishamfunga.
Kwa hakika ni watu wengi wamepata uponyaji, mafanikio, furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, www.kiwangadoctors.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao.
Ommy Dimpoz Amefukuzwa na GSM na kuachishwa Kazi? Aandika haya baada ya tetesi kusambaa
Ommy Dimpoz amefukuzwa na GSM na kuachishwa kazi? Aandika haya baada ya tetesi kusambaa
Thursday, March 20, 2025
JUHIBU Yaja na Mbinu Mpya Kukabiliana na Wanyamapori Waharibifu
Na John Walter -Babati
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (JUHIBU) imeendelea kubuni mbinu mbalimbali za kuzuia wanyamapori waharibifu kuvamia mashamba na kula mazao ya wakulima.
Katika juhudi hizo, JUHIBU imeanzisha matumizi ya baruti, pilipili na mchanga vilivyowekwa kwenye mipira ya kondomu kama moja ya njia za kuwazuia wanyama hao kuingia kwenye mashamba ya wananchi.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 76 vya kuimarisha ulinzi wa mashamba kwa vijiji 10 vya kata ya Mwada, Nkaiti na Magara vinavyohudumiwa na JUHIBU.
Kwa mujibu wa Katibu wa JUHIBU Benson Mwaise, Vifaa hivyo ni pamoja na vilipuzi na honi, ambavyo vinalenga kusaidia wakulima kuwatisha wanyama waharibifu na hivyo kuwaepusha na hasara ya mazao yao.
Amesema kuwa hatua hiyo inalenga kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, hasa katika maeneo yanayopakana na hifadhi za wanyama.
"Tunapenda kuona wakulima wakiendelea kufanya shughuli zao bila hofu ya wanyama waharibifu, huku tukihakikisha kuwa wanyama hawa wanahifadhiwa kwa njia endelevu," alisema Kaganda.
JUHIBU imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta suluhisho endelevu kwa changamoto hiyo, kwa kushirikiana na serikali na wananchi kuhakikisha wanyama na binadamu wanaishi kwa amani bila kuathiri ustawi wa pande zote mbili.
“Hadi Akaanza Kunipapasa Pale Sebleni,” Jamaa Asimulia
Unajua huku duniani kuna matukio ya ajabu sana, unaweza kushangaa na kujiuliza yote haya yanafanyika kwa sababu gani, kwa faida ya nani, na huyu mtu anayefanyiwa hivyo ananufaika na kipi hasa sasa na hapo baadaye.
Jina langu ni Ally kutokea Mombasa ila nyumbani kwa wazazi wangu ni Lamu, mwaka 2021 nilikuja Mombasa kutafuta kazi yoyote ya kufanya maana nilikuwa sijasoma na sina ujuzi wowote ule maishani.
Nilifikia kwa rafiki yangu ambaye miaka ya nyuma tulisoma wote shule ya upili, nilikaa kwake kwa muda wa miezi mitatu hadi nilipopata kazi kwa Baba moja ambaye ni mtu aliyefanikiwa sana kimaisha.
Kusema kweli Bosi huyu alinipenda sana kama mtoto wake maana nilimsaidia sana vitu vingi, umri wake ulikuwa umekwenda ila mke wake alionekana bado ni kijana mbichi, bado alikuwa anatamanisha sana tu.
Walikuwa wanaishi wenyewe tu katika nyumba yao kubwa, hivyo mimi nikawa ni mtu watatu katika familia ile ambayo fedha kwao hazikuwa tatizo kwani watoto wao wanaoishi nje ya nchi walikuwa wanawatumia fedha nyingi za matumizi.
Nilikuwa nafanya kazi yangu ya kutunza bustani nje, kufanya usafi ndani kisha kupika, baada ya hapo nilikaa tu na kutazama tamthilia mbalimbali. Cha ajabu mke wa Bosi wangu wakati mume wake anakuwa hayupo alipenda kuja kukaa wenye sofa ambalo nimekaa na kujikuta tumebanana.
Aliendelea na mtindo huo hadi kuna siku akaanza kunipapasa pale sebleni, hadi akanitamkia kuwa ananipenda sana na analihitaji penzi langu. Nilimwambia siwezi kufanya kitendo kama hicho, basi baada ya siku hiyo akaanza kunichukia na kunileta visa vingi mule ndani.
Asubuhi moja ambayo siwezi kuisahau, nilikamatwa na Polisi na kufikishwa kituo cha Polisi na kuambia usiku wa jana yake nilitaka kumbaka Bosi wangu huyo!. Nilifikishwa mahakamani na kusomewa kesi ya ubakaji, baada ya miezi kadhaa nilipewa dhamana na kuwa nje kwa masharti maalumu.
Nilirejea nyumbani kwa yule rafiki yangu, akaniambia tuwasiliana na mtu anayeitwa Kiwanga Doctors kutokea Migori atatusaidia kwani amewasaidia watu wengi kushinda kesi mbalimbali hasa zile za kusingiziwa.
Basi tulimpigia simu Kiwanga Doctors na kumueleza shida yangu, alinisikiliza kwa makini sana na kunifanyia tiba yake, alinihakikishia baada ya muda sio mrefu nitashinda kesi hiyo, hivyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
Niliendelea kwenda mahakamani kila tarehe ambaye kesi ile ingetajwa, nashukuru kweli niliweza kushinda kesi ile kwa kuonekana sikuwa na hatia yoyote. Sikuweza kuamini daima maana Bosi wangu alikuwa mtu mwenye fedha nyingi, hivyo ingekuwa ni vigumu sana kumshinda katika kesi ile ila nikashinda.
Kwa hakika ni watu wengi wamepata uponyaji, mafanikio, furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao, www.kiwangadoctors.co.tz kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao.
Source
Wednesday, March 19, 2025
DC Babati ataka elimu itolewe kwa wananchi kilimo kisichowavutia Wanyama.
Na John Walter -Babati
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, amewataka watendaji wa maeneo yanayozungukwa na hifadhi kuwapa wananchi elimu juu ya kulima mazao yasiyowavutia wanyama waharibifu ili kuepuka migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.
Kaganda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi magunia 309 ya mahindi kwa vijiji 10 vinavyopakana na hifadhi, mahindi ambayo yamenunuliwa na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (JUHIBU).
Katibu wa JUHIBU, Benson Mwaise, amesema kuwa mahindi hayo yamenunuliwa kwa ajili ya wanachama wa jumuiya hiyo katika vijiji 10 vilivyokubali kuacha kilimo na badala yake kushiriki kwenye uhifadhi.
Mahindi hayo yamegawiwa kwa shule mbalimbali za msingi zilizopo katika kata za Mwada, Nkaiti, na Magara, ili kusaidia chakula cha mchana kwa wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ameagiza wanafunzi waelimishwe kuhusu namna chakula hicho kilivyopatikana, ili wapate uelewa wa umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori na mazingira.
Aidha, Kaganda ameagiza kuandaliwa mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa vijiji vinavyopakana na hifadhi ili kuweka mipaka bayana kati ya shughuli za kilimo na maeneo ya uhifadhi.
Ameeleza kuwa utalii unalipa na wananchi wanapaswa kulima mazao kama tumbaku, ufuta, na aina maalum ya alizeti ambayo hayawavutii wanyama waharibifu.
Pia, amesisitiza umuhimu wa kuweka alama katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya utalii ili kuepusha migogoro, pamoja na kuhakikisha mifugo kama ng'ombe haiingii katika maeneo ya hifadhi.
Mkuu wa wilaya amepongeza JUHIBU, wananchi, na viongozi kwa kazi nzuri ya kusimamia uhifadhi na kuhakikisha jamii inanufaika na rasilimali za wanyamapori kwa njia endelevu.
Diwani wa Nkaiti, Steven Saruni Mollel, amepongeza juhudi za JUHIBU akisema kuwa jumuiya hiyo imeleta manufaa makubwa kwa wananchi, ambao sasa wanaelewa thamani ya uhifadhi.
Amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha jamii kunufaika kupitia rasilimali za wanyamapori.
Hatua ya kugawa mahindi hayo inasaidia wazazi na walezi katika kugharamia chakula cha mchana kwa wanafunzi, hasa kutokana na kupungua kwa shughuli za kilimo kwenye vijiji hivyo kutokana na uwekezaji katika uhifadhi.
Endapo Suala ya Yanga na Simba Litashindikana, Basi Tutawahusisha Serikali...
Source
𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Kifungo cha Paul Pogba Kimeisha na Maisha Yanaendelea Japo Kwa Ugumu
🗣️Paul Pogba: "Pesa hubadilisha watu. Inaweza kuvunja familia. Inaweza kuunda vita. Wakati fulani nilikuwa peke yangu na nilihisi kama sitaki kuwa na pesa tena wala sitaki kucheza tena.
Nilitaka kuwa na watu wa kawaida, kwa hivyo marafiki na familia yangu wananipenda kwa ajili yangu, sio kwa umaarufu, sio kwa pesa."
Paul Pogba Brothers wakiwa na magenge mengine kweli walienda kumuibia, kwa bahati mbaya wezi hao Paul Pogba aliweza kumtambua kaka yake kati yao licha ya yeye kuvaa barakoa (mask) 🎭.
Kwa nini ndugu waligeuka dhidi yake? Sababu ni hii; walihisi Paul hakuwa akiwapa pesa za kutosha licha ya kuwa mmoja wa wanasoka tajiri zaidi duniani, hivyo wakaanza kufanya kila kitu ili kumuangusha Paul Pogba, hata wakatoa siri ya jinsi Paul Pogba alivyoenda Afrika kufanya Voodoo 💔
Baadhi ya wanafamilia ni adui yako mkubwa, kuwa mwangalifu. Mtu anatakiwa kuwa makini sana siku hizi
𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Kifungo cha Paul Pogba sasa ni kimeisha na anapatikana kucheza soka kuanzia leo ✨
Pogba, bado yuko sokoni kama mchezaji huru na yuko wazi kwa ukurasa mpya baada ya mazoezi ya mara kwa mara huko Miami…
Unahisi ni klabu gani inapaswa kwenda kumchukua Paul?
Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Mtandao wa Vodacom M-Pesa
Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Mtandao wa Vodacom M-PesaJinsi Ya
Vodacom M-Pesa inatoa urahisi wa kununua tiketi za mpira bila usumbufu wa foleni ndefu. Ukiwa na simu yako tu, unaweza kupata tiketi yako ndani ya dakika chache. Zaidi ya hayo, huduma hii ni salama, ikilinda taarifa zako za kifedha.
Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Vodacom M-Pesa
Piga *150*00#
Chagua 4 (Lipa kwa M-Pesa)
Chagua 9 (Zaidi)
Chagua 1 (E-payment)
Chagua 1 (Tiketi za Michezo)
Chagua 1 (Tiketi za Mpira)
Chagua mechi unayotaka kulipia
Chagua kiingilio
Weka namba ya kadi ya N-Card
Ingiza namba ya siri
Thibitisha
Exclusive: Mwakinyo Aongea Baada ya Polisi Kumuschia 'Niweke Wazi Hakuna wa Kunihamisha Mtaani Kwangu'
Exclusive: Mwakinyo Aongea Baada ya Polisi Kumuschia, Niweke Wazi Hakuna wa Kunihamisha Mtaani Kwangu
Tuesday, March 18, 2025
Wananchi 7000 Kilosa kunufaika na mnara wa mawasiliano wa Airtel Tanzania
Morogoro, Machi 2025 - Kampuni ya Airtel Tanzania imejenga mnara wa mawasiliano wa 4G Kijiji cha Idete, wilayani Kilosa, Morogoro, ambao unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wapatao 7000, hatua ambayo itawafungulia fursa wananchi hao kunufaika kiuchumi na kijamii.
Akizungumza wakati wa ziara maalumu ya kukagua maendeleo ya ujenzi mnara huo katika Kijiji hicho, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amesema kuwa ujenzi wa minara hiyo iko sambamba na dhamira ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuona Tanzania ya kidjitali na kuona maeneo yote yanafikishiwa mawasiliano.
"Kama alivyosema Mkuu wa Wilaya, kilimo chao wanachokifanya na shughuli zao za kuchunga wanazozifanya wasisumbuke tena kuhangaika kwenda Kilosa mjini. Basi na wenyewe wakae ndani ya mawasiliano waweze kuwasiliana na wateja wao, wauza pembejeo, na waweze kuwasiliana na ndugu zao. Lakini cha muhimu waweze kuwasiliana kama watanzania wengine," alisema Waziri Silaa.
Aliongeza "Lengo hili sisi wasaidizi wa Rais lazima tuhakikishe hili linatimia. Tunataka tarehe moja mwezi wa nne mnara huu uwashwe na tunataka tarehe 15 mnara huu uzinduliwe rasmi na mnara huu uzinduliwe rasmi na mawasiliano yapatikane hapa idete."
Waziri Silaa alisisitiza kuwa mnara huo wa mawasiliano sio tu kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha idete bali ni kwa wananchi milioni 8.5 ndani ya nchi ya Tanzania, akiongeza kuwa kabla ya minara hiyo kujengwa wananchi walikosa mawasiliano, lakini Mheshimiwa Rais alitoa fedha ili wananchi hao waweze kupata mawasiliano.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano kwa Umma wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, alisema kuwa wahandisi wanaojenga mnara huo wameeleza kuwa ujenzi huo unatarajia kukamilika mapema na kuwashwa tarehe moja mwezi Aprili mwaka huu.
"Jambo kubwa ambalo timu yetu ya mauzo imefanya tayari mpaka leo wameshapata mawakala wakubwa watatu ambao ni wakazi wa hapa hapa. Kwa hiyo ni ajira ambayo tumeitoa. Lakini bado pia tumepata mawakala wadogo wadogo ambao wanakuwa wanatoa huduma za Airtel money na Airtel Money branch 10 ambaoi tayari tumeshawasajili na tayari wanangojea mnara ule uwashwe waanze kufanya kazi," alisema Mmbando.
Mmbando aliwataka wananchi kuchangamkia fursa zinazotokana na mnara huo ambao unajengwa kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Monday, March 17, 2025
Asake akubali kuwasaidia Baba pamoja na Mtoto wake baada ya shutuma za kuwatelekeza, Baba ambariki
Asake akubali kuwasaidia Baba pamoja na Mtoto wake baada ya shutuma za kuwatelekeza, Baba ambariki
Tuna Wachezaji Wazawa Wazuri Lakini Tunakosa Mwendelezo wa Ubora, Shida Ipo Wapi?
Sunday, March 16, 2025
ASKOFU MTEULE WA KKKT DAYOSISI YA MWANGA DKT. MONO APOKELEWA KWA SHANGWE KUBWA SHINYANGA

















-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...