
Mti huo, unaomilikiwa na Kanisa la Golan Gospel Center lililopo mtaani hapo, umeibua mijadala kuhusu uwezekano wa tukio hilo kuwa la miujiza.
Baadhi ya viongozi wa kanisa na wananchi wameeleza kushangazwa na hali hiyo.
Katibu wa Kanisa la GGC, Yohana Mathias, amesema tukio hilo limewashangaza waumini wa kanisa na wakazi wa Mpomvu, huku wengine wakilihusisha na nguvu za kiimani.
Mkazi wa Mpomvu, Emmanuel Lameck, amesema hajawahi kushuhudia jambo kama hilo maishani mwake na kwamba bado linafikirisha.
Naye Stella Saimon, mkazi wa Mpomvu, amekiri kuwa tukio hilo limeleta mshtuko kwa wengi, huku wengine wakitafsiri kuwa ni tukio la kiimani au la kishirikina.
Mchungaji wa Kanisa la Golan Gospel Center, Jefta Lameck, amesema mti huo ulikuwa wa muda mrefu, na baada ya kuangushwa na upepo, waliamua kuukata kwa kuwa ulikuwa umezuia njia. Hata hivyo, walipofika asubuhi iliyofuata, walikuta mti huo umesimama tena hali iliyozua mshangao mkubwa.
Amesema tukio hilo lisihusishwe na imani za kishirikina na amewataka wananchi kuwa watulivu huku wakilitafakari kwa mtazamo wa kawaida wa kimaumbile badala ya kuingiza hofu au imani potofu.
Chanzo - Maduka Online Blog