Thursday, February 20, 2025

Mbunge Sillo ampongeza Samia kwa miradi ya Maendeleo



Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Daniel Sillo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Mhe. Sillo ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake katika Kata ya Mamire, ambako alisikiliza kero za wananchi na kueleza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha huduma za kijamii na miundombinu.

Katika ziara hiyo, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mamire na kuahidi kuwa serikali itaendelea kukiboresha zaidi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. 

Pia, ametembelea ujenzi wa ofisi ya Umoja wa Wanawake wa kata hiyo na kuahidi kutoa mifuko 20 ya saruji kusaidia kukamilisha mradi huo.

Mhe. Sillo ameeleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeshatolewa kwa miradi mbalimbali katika kata hiyo, ambapo kati ya hizo, bilioni 3 zimetengwa kwa ujenzi wa geti la kuingilia hifadhi ya Taifa ya Tarangire, jambo linalolenga kuboresha huduma kwa wananchi wa eneo hilo.

Mpaka sasa, Mhe. Sillo amefanya ziara katika kata zote 25 za jimbo hilo na vijiji 102, akisikiliza wananchi na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa ipasavyo kwa manufaa ya jamii.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...