Na John Walter
Mawaziri wa kisekta ambao wanashughulikia masuala ya maafa leo Novemba 17, 2024 wamekutana kwa ajili ya kuendelea na zoezi la uokoaji wa watu waliyokwama kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo kwenye mtaa wa Kongo na Mchikichi.
Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godfrey Mollel, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Khamis na Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga.