Wakati mwingine wanasema ni rahisi kuwa namba moja, lakini ni ngumu kuendelea kuwa namba moja. Kushikilia hapohapo kunahitaji nidhamu na inaonekana hii sio moja ya sifa ya kocha wa Yanga, Miguel Gamondi. Yeye na wachezaji wake wameelekea kushindwa."
"Ukiachana na 'graph' ya mechi ya mtani kuanzia ushindi wa mabao 5-1 mpaka kufikia bao la kujifunga la Kijili, ziko wapi zile bao tano tano ambazo Yanga alikuwa akiwafunga watu pale Chamazi?"
"Kilikuja kisingizio kutoka kwa mashabiki na wachambuzi kwamba timu pinzani zimeisoma Yanga na sasa walikuwa wanakaa nyuma zaidi. Kisingizio cha uongo hicho.
Anasema : Edo Kumwembe.