Saturday, April 18, 2026

CCM Mkoa wa Tanga ya gundua ubadhirifu Saruji 150 ikiwa ni poamoja uwizi wa saruji katika Hospitali ya wilaya Kilindi mkoani Tanga


 Na Rebeca Duwe ,Kilindi


Mwenyekiti wa CCM Mkoa waTanga Rajabu Abdrahman amesema Chama cha Mapinduzi hakitaweza kuwafumbia Macho wale wote wanaohusika na ubadhirifu wa Fedha za serikali kwa kuyafanyia mambo yao binafsi badala ya kufanya kazi iliyo kusudiwa ya kuondoa changamoto za wananchi .


Hayo aliyasema wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Kilindi ambapo kulitokea ubadhirifu wa saruji 145 iliyohifadhiwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ili kuondoa changamoto ya huduma za afya .


Aidha alisema kwa msistizo kuwa amesikia uwizi wa saruji na kuharibika saruji iliyoganda kutokana kukaa kwa muda mrefu bila kutumika kwa kazi iliyokusudia jambo ambalo inaonyesha kuwa ni uzembe wa wataalamu waliopewa kazi hiyo.

"Mradi huu wa Hospitali ya wilaya Kilindi pesa yake imetolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan hivyo kutokutumia ipasavyo ni ubadhitifu wa Pesa za serikali na kuwakosesha wananchi haki zao za kupata huduma ya Afya,kwani kabla ya kutokuwepo kwa Hospitali hiyo wananchi wa Kilindi walikuwa wanaifuata huduma hiyo Morogoro ,Handeni au Tanga mjini jambo ambalo inawatia gharama kubwa ya usafiri wananchi hao."


 Alisema Rajabu

Sambamba na hayo Mwenyekiti huyo CCM aliagiza watu wote waliofanya ubadhirifu kwa njia moja ama nyingine wachukuliwe hatua kali za sheria ili miradi iweze kukamilika kwa wakati kama ambavyo mhe Rais amelekeza na kutaka kuondoa changamoto za wananchi anaowaongoza.


Kwa upande wake MKurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Kilindi mkoani Tanga John Mgalula alisema walipata taarifa za uwizi wa saruji na kumkamata bodaboda akiwa na mifuko mitano ya saruji na kuwapeleka polisi ambapo mpaka sasa kuna mlinzi yuko polisi na fundi pamoja na bodaboda ambapo uchunguzi bado unaendelea kwa mujibu wa taratibu za kisheria.


Aliongeza kuwa baada ya kugundua hivyo walianza kuhesabu na kagundua kuwa kuna mifuko ya aina tatu ambayo ni iliyoibiwa,iliyoganda na ambayo ni mizima ambayo jumla ilikuwa ni mifuko 193 ambayo kuna iliyotumika kati ya hiyo na iliyopo na ambayo imeharibika sana.


Hata hivyo alisema kuwa bado wanaendelea kufuatilia kujua ni mifiko mingapi inafaa na iliyopo ndani ya stoo kwa ujenzi kugundua mifkuko mi ngapi haifai kabisa ili kuendaelea ujenzi Hospitali kwa ajili ya kuwahudumia u wananchi wa kilindi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...