Thursday, October 10, 2024

Dr. Dre afunguliwa kesi ya unyanyasaji

 MAREKANI: Mtayarishaji wa Muziki wa Hip Hop na Rapa, Andre Young maarufu kama Dr. Dre amefunguliwa kesi ya madai ya Fidia ya Dola Milioni 10 (takriban Tsh. Bilioni 27.2) akidaiwa kumfanyia Vitisho na Unyanyasaji aliyekuwa Mshauri na Msuluhishi wa Ndoa yake

Dkt. Charles J. Sophy amedai mwaka 2018, Dr. Dre alianza kumtumia Jumbe za vitisho, Vurugu na Maneno ya Chuki usiku ikiwa ni baada ya kumsaidia kusuluhisha migogoro iliyokuwepo kati ya Dr. Dre na Nicole aliyekuwa Mke wake, kabla hawajapeana talaka

Ndoa ya wawili hao ilivunjika rasmi Desemba 2021 baada ya Nicole kufungua Kesi ya kudai Talaka mwaka 2020 ikiwa ni miaka 24 tangu walipooana. Nicole alimtuhumu Dr. Dre kwa unyanyasaji na kutaka malipo ya zaidi ya Tsh. Bilioni 200.

SOMA :  Mashtaka mapya yamkabili Diddy

The post Dr. Dre afunguliwa kesi ya unyanyasaji first appeared on HabariLeo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...