Thursday, October 10, 2024

Satura: Wasanii hamasisheni uchaguzi mitaa

 MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Jomaary Satura amewahimiza wasanii wa manispaa hiyo kutumia mitandao yao ya kijamii kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Satura amesema hayo Oktoba 10 Dar es salaam alipokutana na wasanii hao ambapo kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa kutaanza Oktoba 11 hadi 20 huku uchaguzi wa serikali za mitaa ni Novemba 27.

SOMA: Tamasha lahamasisha uchaguzi mitaa

Aidha Mkurugenzi huyo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kugombea na kupiga kura ili waweze kupata kiongozi wanaomuhitaji na kuwaletea maendeleo yenye tija kwa jamii.

Satura amesema Halmashauri ya Temeke imeweka vituo zaidi ya 500 vya kujiandikishia ili wananchi wasitembee umbali mrefu na waandikishaji wa vituo hivyo watalala kwenye vituo vyao vya kazi usiiku wa kumakia Oktoba 11 ili kurahisisha kazi kwa wananchi watakaowahi kujiandikisha.

Kwa upande wao wasanii Amani Temba na Deus Mihambo wamesema watatekeleza agizo hilo  la kutumia mitandao ya kijamii kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura uchaguzi serikali za mitaa kwani kuwachangua viongozi wanaowataka watawaletea maendeleo wanayoyataka.

Wamesema wao watakuwa vinara kwa Oktoba 11 kujiandikisha na wataandaa nyimbo ya kuwahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha.

The post Satura: Wasanii hamasisheni uchaguzi mitaa first appeared on HabariLeo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...