Wednesday, August 14, 2024

Hawa VitalO Wanautani wa Ngumi na Yanga, Eti Wadai Wamekuja Kuwatoa Yanga



Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa time ya Vital'O ya Burundi Arsene Bucuti amesema wamekuja nchini kuitoa Yanga SC Katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Vital'O imepangwa kucheza na Yanga SC patika Mashindano ya klabu Bingwa Afrika na mchezo huo utafanyika Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi.


Arsene alisema wanaiheshimu Yanga SC lakini hiyo haiwafanyi waihofie na wamekuja Tanzania kwa ajili ya kazi hiyo ya kuwatoa kwa kuwa wameifuatilia vyema.

"Tumekuja hapa kwa kazi moja tu. Kuwatoa Yanga SC tuna kila kitu ambach wao wameshinda hatutishiki nao.


"Tumewafatilia Katinka michezo Yote ambayo wamecheza kule Afrika Kusini hadi hapa Tanzania hivyo tunaenda kucheza na timu tunayoifahamu vyema" Yanga ina mashabiki Burundi??


"Ndiyo Yanga SC ina mashabiki wengi Burundi kutokana na wachezaji Ammis Tambwe, Saidoo Ntibazonkiza na Didie Kavumbagu kuwahi kuiumikia timu hiyo", alisema Arsene Bucuti.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...