Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa kulikumbatia katika biashara yako ni, kuelewa mbinu za kufanya biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa wenzetu wazungu mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia kutengeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani.
Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi dunia ya sasa inakwenda kasi sana tofauti na ilivyokuwa nyuma.
Na ili uweze kwenda sawa na kasi hiyo ni lazima jifunze mbinu mbalimbali zitakazokusaidia kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwani kwa sasa wanaitumia njia hiyo ndiyo ambao wanafaidi matunda ya kutumia mbinu hizo.
Jambo jingine ambalo litaweza kukusaidia kuweza kuongeza mauzo ya katika biashara unayoifanya ni kuhakikisha unakuwa mtalamu katika biashara husika. Hii mbinu muhimu sana katika kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara kwa sababu pindi utakapokuwa mtalamu au m-bobezi wa jambo hilo itakusaidia sana kuweza kuizungumzia vizuri bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja wako, kufanya hivyo kutamfanya mteja huyo ainunue bidhaa hiyo. Hivyo ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara yako jifunze kuwa mtalamu katika eneo husika unalolifanya.
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu sana litakalo kusaidia kuweza kufanya biashara yenye tija ni kuhakikisha unaimarisha vizuri upande wa huduma kwa mteja, kwa sababu ule usemi wa kwamba mfalme ni mteja hakuwepo tu, bali msemo huo upo kumanisha kweli, mteja ni mfalme pindi awapo na asipokuwapo katika eneo lako la kibiashara pia.
Ufike pahala neno mteja liwe lina maana kubwa sana katika biashara yako, yaani mfanye mteja kuwa ni sehemu ya biashara ya yako. Mfanye mteja ajisikie huru katika suala zima la kibiashara.
Mwisho nimalize kwa kusema biashara yenye tija hujengwa na vitu vitatu vya msingi ambavyo ni bidhaa au huduma nzuri+ masoko mazuri= wateja wengi.
Na. Benson Chonya