Tuesday, June 1, 2021

Ujerumani yaanzisha uchunguzi kwenye vituo vya kupima Covid-19


Uchunguzi umeanzishwa nchini Ujerumani juu ya madai ya udanganyifu katika vituo vya kupima virusi vya corona (Covid-19) ambapo vipimo vya haraka hufanywa bila malipo.

Kulingana na ripoti kwenye vyombo vya habari vya Ujerumani, vituo vingine vya kupima vilionyesha idadi ya vipimo walivyoripoti kwa mamlaka husika zaidi ya vile vilivyokuwa halisi.

Katika ripoti hiyo, ilisemekana kwamba baadhi ya vituo vya kupima katika miji ya Cologne, Münster na Essen na katika jimbo la Bavaria viliwasilisha idadi ya vipimo kwa mamlaka husika bila kutoa ushahidi wowote na kupokea pesa kutoka kwao.

Ilielezwa kuwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi ya mwendesha mashtaka ilianzisha uchunguzi dhidi ya watu kadhaa kwa tuhuma za udanganyifu.

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn alisisitiza kwamba vituo vya kupima vinapaswa kuchunguzwa na mamlaka za afya za serikali za mitaa na kusema,

"Serikali ya shirikisho inaweka mfumo, inatunga sheria na inalipa gharama, lakini serikali haiwezi kukagua mitandao ya vipimo kwenye tovuti."

Spahn aliongezea kusema kuwa atajadili suala hilo na mawaziri wa afya wa serikali.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...