Wednesday, June 2, 2021
RC Kafulila aanza kwa kuzichimbua fedha za madini ya ujenzi.
Samirah Yusuph
Simiyu. Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila ameagiza uhakiki wa kiasi cha madini ya ujenzi yanayotoka katika kila halmashauri za wilaya ya mkoa huo kwenda katika ujenzi wa barabara na miradi mingine.
Agizo hilo amelitoa Juni 1,2021 alipo kuwa katika ukaguzi wamradi wa ujenzi wa Barabara ya Bariadi, Mwigumbi yenye urefu wa kilometa 50.3 kufuatia uwepo wa halmashauri za wilaya ambazo hazifahamu thamani ya malipo ya madini hayo.
Kafulila ameagiza kuwa kila halmashauri kufanya uhakiki wa kiasi cha madini ambayo yamechimbwa kwa kipindi cha miaka mitano na kupata thamani yake ili mkandarasi aliyehusika na uchimbaji huo afanye malipo.
"Halmashauri zote ndizo zenye mamlaka ya kutenga maeneo ya kuchimba madini ya ujenzi na walipwe ushuru wao, ili pesa ya Mrahaba na asilimia moja ya ukaguzi iende tume ya madini...Ile dhana ya mtu kuendelea kuvuna kokoto kwa leseni ya Tanroad baada ya kuwa mradi umekamilika iwe ni mwisho".
Aidha ameongeza kuwa hadi sasa Tume ya madini mkoa wa Simiyu inadai tsh670 milioni za mirahaba ya madini kwa mkandarasi wa barabara hiyo huku pesa iliyolipwa kwa kipindi chote hicho ikiwa ni tsh 20 milioni pekee huku halmashauri ya wilaya ya Maswa yalipo machimbo ya kokoto hizo haifahamu ni kiasi gani inatakiwa kulipwa.
Jambo ambalo mkurugenzi wa wilaya hiyo Dkt Fredrick Sagamiko ameelezea kuwa licha ya halmashauri kufuatilia kwa ukaribu zoezi la uchimbaji wa madini hayo kwa kipindi chote hawakuweza kupewa ushirikiano na wakala wa barabara (tanroads) ambaye ndiye mwenye mkataba na mkandarasi.
Katika hatua nyingine Kafulila amewatahadharisha wakandarasi wanaofanya kazi chini ya kiwango katika mkoa huo kuwa hakuna nafasi ya kuwavumilia tena huku akimtaka mkandarasi anayejenga kipande hicho cha barabara kufanya kazi kwa weredi baada ya kazi ya awali kulazimika kuirudia kutokana na kuwa ilijengwa chini ya kiwango ujenzi ambao umeanza tangu 2015 hadi sasa haujakamilika.
Mwisho.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...