Na Maridhia Ngemela
Wafanya biashara wameshauriwa kuendelea kulipa kodi ili kuendeleza maendeleo mbalimbali ambayo yananufaisha wananchi.
Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mwanza (TRA) imewataka Wafanyabiashara kuzingatia wakati wa kufanya makadirio ya kodi Kwa kufuata Sheria na kanuni zilizopo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msimamizi wa Idara ya Elimu ya mlipa kodi Mkoani hapa Lutufyo Mtafya amesema uzingitiaji wa Sheria ya kodi kwa muda muafaka ili kuepukana na usumbufu ambao unaweza kusababisha kufungwa kwa biashara.
Anaeleza kuwa ukadiriaji wa kodi kwa wakati kunaepusha mlundikano wa foleni bila kuathiri utendaji wa Kazi.
Amesema Mfanyabiashara ana wajibu wa kutoa taarifa zake za kodi ambapo itarahisisha utambuzi wa biashara bila kuwa na hasara.
Aidha amesema Wafanyabiashara wenye mitaji kidogo wanaruhusiwa kutumia vitambulisho kwa matumizi ya TRA.
Hata hivyo mmoja wa wafanya biashara wenye mitaji midogo midogo Maimuna Saleh wa mkoani hapa ameeleza kuwa walipewa taarifa na ofisi ya kata kuwa wanatakiwa kuwa na leseni za biashara na sio vitambulisho.