Saturday, May 8, 2021
Waziri Mulamula Akutana Na Mabalozi Wanne, Kupokea Nakala Ya Hati Ya Utambulisho
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kuzungumza na mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na kupokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji hapa nchini.
Mabalozi waliokutana na Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba, Balozi wa Indonesia Mhe. Ratlan Pardede, Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Mulamula na mabalozi hao wamejadili juu ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano baina ya mataifa wanayoyawakilisha hapa nchini na Tanzania.
"Leo nimekutana na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, akiwemo Balozi wa Rwanda, Sweden, Norway na pia nimepokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji na kuwahakikishia ushirikiano wetu kama wizara, kama nchi katika kuboresha na kukuza mahusiano yetu," amesema Balozi Mulamula
Nae Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda ni mzuri hivyo wataendelea kuudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.
"Nchi zetu mbili zimekuwa zikishirikiana vizuri hivyo tumekubaliana kuendelea kudumisha ushirikiano huu kwani Watanzania na Wanyarwanda ndugu na marafiki," amesema Balozi Karamba
Kwa upande wake Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede amesema Indonesia na Tanzania zitaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uchumi, utalii na kijamii na kuhakikisha kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika.
"Tumejaribu kuwahamasisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza hapa Tanzania na hadi sasa kampuni kumi (10) zimewekeza katika sekta za biashara na uwekezaji, madini, uvuvi, ujenzi na viwanda," amesema Balozi Pardede
Nae Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg amesema kuwa Sweden itaendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki za binadamu.
"Tumejadiliana kuhusu kuimarisha mahusiano, biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira pamoja na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu," amesema Balozi Sjöberg.
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema Norway na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri ambapo kwa sasa Norway inaangalia fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini ili kuimarisha mahusiano na kukuza uchumi.
"Norway itaendela kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Tanzania ili kuimarisha mahusiano yetu na kukuza uchumi wa pande zote mbili," amesema Balozi Jacobsen
Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
