Saturday, May 8, 2021

Watu wengine zaidi wafariki kwenye maandamano ya kupinga mageuzi ya ushuru nchini Colombia

Idadi ya vifo katika maandamano ya kupinga mageuzi ya ushuru ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku 9 nchini Colombia iliongezeka hadi 26.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Ombudsman ya Colombia, ilitangazwa kuwa idadi ya vifo katika maandamano ya kupinga mageuzi ya ushuru ambayo yalianza mnamo Aprili 28 imeongezeka kutoka 24 hadi 26.

Imeripotiwa kuwa kesi za kupotea kwa watu 55 kati ya 145 hadi sasa zimepatikana, na uchunguzi unaendelea kwa watu 90.

Waziri wa Kazi wa Colombia Angel Custodio Cabrera alisema serikali iko tayari kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Kamati ya Maandamano ya Kitaifa kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa.

Cabrera alitangaza kuwa mkutano huo, uliopangwa kufanyika Mei 10 kati ya Rais Ivan Duque na wawakilishi wa Kamati ya Maandamano ya Kitaifa unaweza kufanyika haraka iwezekanavyo, na mrengo wa serikali ulikuwa tayari kwa hili.

Cabrera pia alitaka kukomeshwa kwa vitendo vyote vya vurugu kwenye maandamano hayo.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...