Tuesday, April 20, 2021
Naibu Waziri Masauni Awataka Vijana Kuchangamkia Fursa Za Uchumi Wa Blue Zanzibar
Na Benny Mwaipaja, Zanzibar
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewahimiza vijana Visiwani Zanzibar kuchangamkia fursa za uchumi wa blue unaotokana na shughuli za uvuvi na uchakataji wa samaki ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Masauni ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar, ametoa rai hiyo wakati akizungumza na viongozi na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kikwajuni akiwa katika ziara yake ya kikazi visiwani humo.
Amesema kuwa yeye binafsi na Mwakilishi wa Jimbo hilo katika Baraza la Wawakilishi Mhe. Nasor Ali Jazeerah pamoja na viongozi wengine wamejipanga kutoa vifaa vitakavyotumiwa na vijana kwa ajuili ya shughuli za uvuvi katika sekta hiyo ya uchumi wa blue ili waweze kujitegemea kwa kujipatia kipato cha uhakika.
"Tunataka tuangalie uwezekano wa kujenga mazingira mazuri ya kuwatafutia "ndoano" na siyo "samaki" na tumeandaa vitu vikubwa ambavyo sitaki niseme mapema hapa nitaondoa radha, mkawaambie vijana wa Kikwajuni kama hawatatoka kimaisha kipindi hiki hawatatoka maisha" alilisisitiza Mhe. Masauni.
Pamoja na kusisitiza masuala ya kiuchumi, Mhandisi Masauni alisema kuwa mipango mingine iliyowekwa na uongozi katika Jimbo la Kikwajuni ni kuendesha mashindano ya kusoma qoran kwa vijana na kuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki mashindano hayo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nasor Ali Jazeerah, aliwaahidi wakazi wa Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar kwamba ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita zitatekelezwa kikamilifu.
Alitoa wito kwa wakazi wa Jimbo hilo kushikamana, kupendana na kuacha majungu ili mipango ya maendeleo iliyopangwa iweze kutekelezwa kwa kasi zaidi.
Aliwashukuru wananchi kwa kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ili waendelee kuingoza nchi kwa umahili mkubwa.
Mwisho.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
