Sunday, March 14, 2021
VIONGOZI SIMIYU WAASWA KUTUMIA BUSARA BADALA YA NGUVU
Na Stella Kalinga, Simiyu RS.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Serikali mkoani hapa kutumia busara na akili badala ya kutumia nguvu katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo waliyopo na kuhakikisha ufumbuzi unaotolewa unaleta tija kwa wananchi.
Mtaka ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao maalum cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) , kilichofanyika Machi 13, 2021 Mjini Bariadi kwa lengo la kupitia Rasimu ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Simiyu ya mwaka 2021/2022.
"Wito wangu kwa viongozi wenzangu tupunguze kutumia nguvu, tuongeze matumizi ya akili tuone matokeo kwa wananchi wetu, leo tunapitisha mapendekezo ya bajeti ya mkoa mwaka 2021/2022 lakini ningetamani kuona miradi mipya ya Halmashauri inayogusa watu, halmashauri zetu zijielekeze kwenye kuanzisha miradi ambayo itakuwa vyanzo vipya vya mapato," alisema.
Aidha, Mtaka ametoa rai kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri kupima tija ya vikao vyao na kuhakikisha vikao wanavyokaa vinaleta tija ikiwa ni pamoja na namna vikao hivyo vinavyosaidia kubuni na kuongeza vyanzo vya mapato.
Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti ya Mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi-Sehemu ya Mipango na Uratibu, Bw. Donatus Weginah amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Simiyu inatarajiwa kutengewa shilingi bilioni 200.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, mishahara na matumizi mengineyo.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa ameunga mkono mapendekezo ya mpango na bajeti ya mkoa na kuahidi ushirikiaono wa wabunge hao katika kupitisha bajeti hiyo bungeni.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa kwa viongozi wote mkoani Simiyu kushirikiana na vyombo vinavyohusika na usimamizi wa fedha kudhibiti na kusimamia matumizi ya fedha zote za Serikali ili ziweze kuleta tija.
Akitoa salamu kwa naiba ya Chama cha Mapinduzi, Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu, Bi. Haula Kachwamba amewashauri wataalam kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kubuni vyanzo na mbinu za kuongeza mapato kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mkoa wa Simiyu .
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
