Sunday, March 14, 2021

Ninja Asimulia Magumu Wanayopitia Yanga SC




BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' amefunguka kwamba wamekuwa wakipitia wakati mgumu kutokana na safu yao ya ulinzi kuruhusu mabao mara kwa mara katika michezo ya Ligi Kuu Bara jambo lililovuruga mipango yao.

 

Ninja ambaye amekuwa hana nafasi kubwa ya kucheza ndani ya Yanga msimu huu, ametoa kauli hiyo kufuatia hivi karibuni timu yao kuwa na matokeo yasiyoridhisha ikiwemo kupoteza mbele ya Coastal Union na sare dhidi ya JKT Tanzania.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ninja alisema: "Mashabiki wanatakiwa kufahamu kwamba bado tupo katika mbio za ubingwa, hivi sasa tumeyumba kwa kuwa tumekubali kuruhusu mabao katika baadhi ya mechi zetu za hivi karibu na kuvuruga mipango mingine."

 

Bado tunaamini tuna nafasi ya ubingwa kwa kuwa hakuna timu ambayo hadi sasa ina uhakika, sisi ndiyo tunaongoza ligi."Watu wanasema kwa nini timu haifungi mabao, ila ukweli ni kwamba mabao yanafungwa, angalia mechi dhidi ya Kagera, tulifunga mabao mengi, ila tatizo lilikuwa kwenye safu ya ulinzi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...