Wednesday, March 31, 2021

Poshy: Uzazi Umeniongezea Mvuto





MREMBO ambaye umbo lake lilimfanya kumpa jina kubwa hapa mjini, Jacqueline Obadia 'Poshy' amesema kuwa tangu amejifungua mtoto wake, amezidi kuwa mrembo tofauti na hata alipokuwa hajajifungua.

Akizumgumza, Poshy alisema kuwa watu wengi wanadhani kuwa unapopata mtoto mwili unaharibika lakini ukweli ni kwamba ukizaa na ukajikubali mwili unakuwa mzuri na unaongezeka mvuto.



"Toka nimejifungua kwa kweli naona kabisa mvuto umeongezeka sana maana wengine walikuwa wanasema kuwa ukijifungua utaharibika lakini ukweli ni kwamba tangu nijifungue nimezidi kuwa bomba sana na ninavutia tofauti hata na mwanzo," alisema Poshy.

Stori na Imelda Mtema | GPL

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI...AONYA DHARAU KAZINI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Na Damian Masyenene
KUFUATIA Uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na kumteua Katibu Mkuu Kiongozi mpya.

Rais Samia ametangaza mabadiliko hayo leo saa 9 Alasiri katika hafla ndogo ya kumuapisha Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Katika uteuzi huo, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi wa Tanzania nchini Japan, Hussein Yahya Katanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.

Kwa upande wa mabadiliko ya baraza la mawaziri, Rais Samia Suluhu Hassan amemhamisha aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Seleman Jaffo akipelekwa kushika nafasi ya Ummy Mwalimu.

Mwigulu Nchemba amepelekwa wizara ya Fedha na Mipango akisaidiwa na Hamad Masauni na nafasi yake katika Wizara ya Katiba na Sheria kuchukuliwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akisaidiwa na Jofrey Mizengo Pinda.

Balozi Liberata Mulamula ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, huku naibu wake akiteuliwa Mbarouk Nassoro Mbarouk.

Kwa upande wa Wizara ya Nchi ofisi ya Rais, utumishi na Utawala bora, ameteuliwa Mohamed Omary Mchengelwa, huku aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Capt. George Mkuchika akipangiwa kazi nyingine.

Wizara ya Uwekezaji imerejeshwa katika ofisi ya Waziri Mkuu na kutolewa ofisi ya Rais, huku Geoffrey Mwambe akiteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo na Prof. Kitila Mkumbo akipelekwa wizara ya Viwanda na Biashara.

Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa wizara ya Michezo, Sanaa, Utamaduni na Michezo, huku aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo, Abdallah Ulega akipelekwa wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa naibu waziri.

Naye, Mwanaidi Ally Hamis ameteuliwa kuwa naibu waziri wa pili katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 

Akitangaza mabadiliko hayo, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuondoka kwa Dk. Philip Mpango katika Wizara ya Fedha na Mipango kumempa nafasi ya kulitazama baraza lote la mawaziri na kufanya mabadiliko kidogo.

"Nimeona niwabadilishe kwa sababu tangu mumeapa ni muda mfupi kuona nani ameshindwa, tunaanza na hawa awamu ya sita, jinsi tunavyokwenda tutaona nani tunakwenda nae na nani tunamuacha.

"Naibu mawaziri mkatumike vizuri, kuna kudharauliana, naibu anadharau waziri na waziri nae anadharau naibu, kazi ni kazi sitaki kusikia kingine," amesisitiza.

Katika upande mwingine, Rais Samia amefanya uteuzi wa wabunge watatu ambao ni Dk. Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk

Via Shinyanga Press Club  blog

RAIS SAMIA AMTEUA BALOZI YAHAYA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI KUCHUKUA NAFASI YA DK. BASHIRU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Yahaya Katanda kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.

MCHINA AKAMATWA KWA KUWACHARAZA VIBOKO MADEREVA WAILI


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia raia wa China Xiao Yong (33) kwa tuhuma za kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko madereva wawili kwa madai ya kutumia fedha walizopatiwa kupeleka wilayani Kyela kwenye mashine za mchezo wa kubahatisha.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Urlich Matei jana Jumanne Machi 30, amewataja walioshambuliwa kwa viboko na kusababishiwa maumivu makali kuwa ni Ramadhani Ulodi (27) na Omary Miraji 25).

Amesema awali jeshi lilipata taarifa kutoka katika mitandao ya kijamii zikionyesha raia wa Tanzania wakichalazwa viboko na ndipo walipanza kufuatilia na kubaini lilitokea katika Mtaa wa Meta, Kata ya Mabatini Jijini hapa.

"Tulianza ufuatiliaji na kubaini Watanzania hao ambao ni waajiriwa wa Kampuni ya Bonanza,"amesema.

Matei amesema polisi hawajafurahishwa na kitendo hicho na kuonya raia wa kigeni kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga waajiriwa wao badala yake wawafikishe katika vyombo vya dola.

Amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi na atafikishwa mahakamani uchunguzi wa kesi hiyo utakapokamilika.

CHANZO - GLOBAL PUBLISHERS

BLOGGER SHAMIMU MWACHA NA MMEWE WATUPWA JELA MAISHA


Mahakama Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imemhukumu blogger Shamimu Mwasha (41), na mume wake Abdul Nsembo, maarufu kama Abdulkandida (45) kutumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hukumu hiyo imetolewa leo Machi 31, 2021 na Jaji Elieza Luvanda baada yaa kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi sita wa upande wa mashtaka.

Shamimu anayemiliki Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, walikuwa wanakabiliwa na
mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 439.70, kosa wanalodaiwa kulitenda Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

CHANZO- MICHUZI BLOG

AJALI YA BASI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI 19

Watu sita wamefariki dunia na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Machame Investment lililokuwa likitoka jijini Dodoma kwenda Moshi kupata ajali kwenye kijiji cha Kiongozi wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishina Msaidizi Mwandamizi Paul Kasabago amesema uchunguzi wa awali wa ajali hiyo iliyotokea Jumanne Machi 30,2021 unaonyesha chanzo ni mwendo kasi.

Huu ndio MJENGO anaoishi ZUCHU, sio mchezo, aweka vdeo hii kuuonesha kwa mara ya kwanza

 


Huu ndio MJENGO anaoishi ZUCHU, sio mchezo, aweka vdeo hii kuuonesha kwa mara ya kwanza

VIDEO:

Tuesday, March 30, 2021

Ufafanuzi kuhusu utata wa kauli ya MO Dewji




Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya klabu ya Simba, Mulami Ng'ambi amefafanua ujumbe wa mkurugenzi wake wa bodi, Mohammed Dewji baada ya kutwitt na kueleza hisia zake juu ya uwekezaji wa mkataba mpya wa klabu ya Manchester United na kuhusisha Simba na mkataba wa Sportspesa.


MO aliandika, "Man utd italipwa kiasi cha pauni milini 305 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 700 za kitanzania kwa miaka mitano kutoka kwa (Team Viewer).

.

Simba ya Tanzania haipati hata asilimia moja ya hiyo pesa kutoka kwa wadhamini Sportpesa (Asilimia moja ya hiyo pesa ni kiasi cha Bilioni 7 za kitanzania)."



Mulami amefafanua ujumbe huo kupitia East Africa redio kwa kusema,''Watu hawakumuelewa Mo Dewji''Mulamu Ng'ambi.



''Alichokimaanisha Mohamed Dewji alikuwa anaamnisha kwamba, hela ambayo ipo au inawekezwa kwenye mpira kama udhamini bado ni kidogo sana kulinganisha na nchi nyingine ambazo zinapata udhamini''.



''Nafkiri alisema Simba haipati asilimia moja ya udhamini ambayo Manchester United wanaipata katika mkataba mpya ambao wameisaini hivi karibuni.''



''Manayake ni kwamba ilikuwa ni kuhamasisha makampuni juu ya umuhimu wa kuongeza fedha zao kwenye mpira.''



''Hakuwa akimaanisha ni Sportpesa pekeyake, ikumbukwe kulikuwa na makampuni mengi ambayo yalijiondoa katika mpira wetu,NMB, TBL na zaidi.''



''Ukweli ni kwamba fedha inayowekezwa kwa sasa ni ndogo sana ikilinganishwa na thamani ya Simba iliyonayo hivi sasa.''



''Ni kweli kwamba kutokana na makubaliano ya kipindi hicho na ni sahihi kwa kipindi hicho Sportpesa walikuwa wakombozi wa vilabu vyetu kwasababu TBL walijiondoa hivyo walitusaidia, lakini uhalisia kwasasa kuna haja ya kutafakari upya.''



''Mtu ambaye tunafanya naye kazi ndiye anapewa kipaumbele katika makubaliano ya mkataba mpya ili kuboresha.''



''Iwapo hakutokuwa na maslahi, ni bora hata utoe nafasi bure kusaidia jamii kuliko kuendelea kutangaza na kupokea kiasi ambacho hakiendani uhalisia wa thamani ya klabu yetu"



Mulamu Ng'ambi-Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba akizungumza na David Kampista-East Africa Radio.

Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti na Katibu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Florencs Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma akichukua nafasi ya Dkt. Charles Msonde ambaye amemaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Mhandisi Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) akichukua nafasi ya Prof. Patrick Makungu ambaye muda wake umekwisha, mwingine aliyeteuliwa ni Dkt. Blandina Lugendo ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) .

Rais Samia pia amemteua Paulina Nkwama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, kabla ya uteuzi Nkwama alikuwa Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) Mkoa wa Kilimanjaro na anachukua nafasi ya Winfrida Rutaindurwa ambaye amemaliza muda wake.



Kila nikikumbuka Sauti ya Dkt. Magufuli natoka machozi- Wastara





Msanii wa Bongo Muvi Tanzania Wastara Leo afunguka namna alivyopokea kifo cha Hayati JPM akiwa Nyumbani kwake
 "Nakumbuka Mwaka 2018 Hayati JPM alinipigia simu nikiwa Nyumbani kwangu nikiwa sijiwezi Ni Mtu wa kulala Muda Wote nikiwa naugulia Mguu wangu".

Dkt.Magufuli Alinipa Moyo nizidi kumuomba mungu Ili anifanyie Wepesi nipone Haraka.

"Kila nikikumbuka Sauti ya Dkt. MAGUFULI natoka machozi maana Alikuwa anazungumza na mimi kama Baba yangu Mzazi".

"Ninachoniuma Zaidi Baadhi ya WASANII Wananichukia Nahisi ni kwa vile Viongozi wa Nchi yetu Wananisaidia kila ninapopata Matatizo"

Picha : JIELONG HOLDINGS LTD, KANISA LA BAPTISTI WAKABIDHI MADAWATI SHULE ZA KIZUMBI..DC MBONEKO AAGIZA WATORO WAFUATILIWE

Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40,viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekabidhi madawati, meza na viti vyenye thamani ya shilingi milioni 3.5 yaliyotolewa na Kiwanda cha mafuta ya kula cha Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende kwa ajili ya shule ya msingi Kizumbi na shule ya Sekondari Kizumbi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Mhe. Mboneko amepokea meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021.

Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi meza 40, viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya shule ya Sekondari Kizumbi vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.1 na madawati sita yenye thamani ya shilingi laki 4 kutoka Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu kwa ajili ya shule ya msingi Kizumbi.

Akizungumza, Mboneko ameishukuru Kampuni ya Jielong Holdings (T) LTD na Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu kwa mchango wao katika sekta ya elimu kwa kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa viti na meza pamoja na madawati katika shule ya msingi Kizumbi na shule ya sekondari Kizumbi.

"Tunawashukuru wadau wetu kwa kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutupatia meza,viti na madawati. Suala la kuboresha miundombinu ya shule ni la kila mtu,naomba wadau wengine,wawekezaji wengine waliopo ndani na nje ya wilaya ya Shinyanga wajitokeze kusaidia ili tumalize changamoto zilizopo katika shule mbalimbali ili watoto wetu wasome katika mazingira bora",amesema Mboneko.

"Sisi serikali kazi yetu ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri, wazazi kuhimiza watoto waende shule na kuwapatia mahitaji muhimu nanyi wanafunzi kuhakikisha mnasoma kwa bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zenu ikiwemo kupata ujauzito mngali wanafunzi",ameongeza Mboneko.

Mboneko ametumia fursa hiyo kuwapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwashukuru walimu watano wanaojitolea kufundisha katika shule ya sekondari Kizumbi.

Katika hatua nyingine amesema suala la utoro kwa wanafunzi halikubaliki hivyo amewaagiza walimu ,wazazi na viongozi wa idara ya elimu katika wilaya ya Shinyanga kufuatilia wanafunzi watoro warudishwe shuleni kuendelea na masomo.

Pia ametoa taarifa ya serikali kuleta fedha shilingi milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule ya  Sekondari Kizumbi na shilingi milioni 12.5  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa katika shule ya msingi  Bugayambelele iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji amesema wamechangia viti,meza na madawati ili kushirikiana na serikali katika kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu amesema wameamua kuchangia madawati katika shule ya msingi Kizumbi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea na kukabidhi meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Doris Dario, kushoto ni Mkuu wa shule ya sekondari Kizumbi, Marco Msangwa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea na kukabidhi meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatunza meza,viti na madawati yaliyotolewa na wadau.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akizungumza wakati akikabidhi meza 40,viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mfanyakazi wa kiwanda hicho Bi. Khadija Yusuph akitafsiri lugha ya Kichina kwenda Kiswahili.
 Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu akizungumza wakati akikabidhi madawati sita kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40 na viti 40 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40 na viti 40 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye meza 40 na viti 40 vilivyotolewa na Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati 10 yaliyotolewa na Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 6 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 6 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati 6 yaliyotolewa na Kanisa la Baptisti kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akiwataka wanafunzi katika shule ya msingi na sekondari Kizumbi kutunza viti, meza na madawati.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akiwataka wanafunzi katika shule ya msingi na sekondari Kizumbi kusoma kwa bidii na kuepuka utoro shuleni.
Wazazi, walimu na wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza wakati zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Mkuu wa shule ya sekondari Kizumbi Marco Msangwa akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati ambapo alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 601, ilikuwa na upungufu wa madawati/viti na meza  460 na baada kupokea viti 40, meza 40 na madawati 10 sasa wana uhaba wa viti 19 na meza 19.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kizumbi Joshua Masengwa akisoma taarifa ya kata  wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Doris Dario akizungumzma wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Mwenyekiti wa CCM kata ya Kizumbi, Kudililwa Ndimila akizungumza wakati wa  makabidhiano ya meza,viti na madawati
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.

Beyonce Avamiwa na Majambazi, Waondoka na Mzigo wa Mabilioni


Beyonce ni muhanga wa tukio la uvamizi, avamiwa na kuibiwa vitu vyenye thamani ya ($1 million) takribani TSh. Bilioni 2. Kwa mujibu wa taarifa toka mtandao wa TMZ, wezi hao walifanikiwa kuvamia eneo/nyumba ambayo Beyoce huwa anahifadhia mali zake ikiwemo vito vya thamani mjini Los Angeles.


Imeelezwa, wezi hao walifika na kuiba zaidi ya mara mbili kwenye maghala hayo mwezi huu. Awamu ya kwanza, waliondoka na vitu kama pochi na magauni ya thamani. Awamu ya pili walirejea na kuiba pochi, midoli ya watoto na picha.


Eneo hilo limekodishwa na kampuni ya Beyonce iitwayo Parkwood Entertainment na hutumika kuhifadhia vifaa vya production na vitu vingine binafsi vya Beyonce. Polisi wanaendelea na uchunguzi na hadi sasa hakuna aliyekamatwa.

Kama nilimkwaza mtu mnisamehe, Mimi ni binadamu- Dkt. Philip Mpango







"Mimi ni binadamu pamoja na kwamba mmesema maneno mazuri juu yangu mengine hamkusema nataka nitumie nafasi hii pale ambapo nilimkwaza mtu yoyote, mhe. Mbunge yeyote humu ndani au nje katika nafasi yangu ya Waziri wa Fedha na Mipango naomba mnisamehe" Makamu wa Rais wa Tanzania Mteule, Dkt. Philip Mpango

BUNGE LAMTHIBITISHA DR MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dr. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 100%.

Wabunge 363 wote waliokuwepo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 wamepiga kura za NDIO kumthibitisha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Dkt. Mpango amethibitishwa baada ya kupendekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan na jina lake kusomwa bungeni mjini Dodoma na Spika Job Ndugai.

"Naomba kutangazia Bunge hili na nchi yetu kwa ujumla kwamba kura za hapana hakuna hata moja, kura zote 363 ni kura za ndiyo kwa hiyo amepata asilimia 100 ya kura zote",amesema Ndugai.

Rais Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Philip Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya leo Jumanne na mpambe wa Rais katika bahasha maalum.

WHO: Huenda COVID ilitoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu




Ripoti ya pamoja ya shirika la afya duniani WHO na China kuhusu chanzo cha mlipuko wa COVID-19, inaonyesha kwamba maambukizi kutoka kwa popo kwenda kwa binadamu huenda yalipita kwa mnyama mwingine na sio kutoka maabara. 

   
Ripoti ya pamoja ya utafiti wa shirika la afya duniani WHO na China kuhusu chanzo cha mlipuko wa COVID-19, inaonyesha kwamba maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa popo kwenda kwa binadamu huenda yalipita kwa mnyama mwingine na sio kutoka maabara. 

Utafiti huo hata hivyo umetoa mwangaza kidogo wa jinsi gani mlipuko huo ulianza na unaacha maswali mengi bila ya majibu, lakini ripoti hiyo imetoa maelezo ya kina kwanini watafiti wamefikia hitimisho hilo.

Timu ya watafiti imependekeza utafiti zaidi katika kila eneo kasoro katika nadharia ya kwamba virusi hivyo vilianzia maabara, dhana ambayo iliwahi kuelezwa na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuwa miongoni mwa sababu za mlipuko wa virusi vya corona.

Pia inasema kwamba dhana ya virusi hivyo kusambaa kupitia soko la vyakula vya baharini katika mji wa Wuhan  China ambako kisa cha kwanza kiligundulika, haikuwa na uwezekano mkubwa. Ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kuwekwa hadharani hii leo, inatazamwa kwa ukaribu na wanasayansi wanaojaribu kufahamu chanzo cha mlipuko wa COVID-19 ili kuweza kuzuia magonjwa ya milipuko ya baadae, lakini pia imekuwa nyeti kwa China ambayo inadai kuwa haipaswi kulaumiwa kwa mlipuko huo.

Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza wa Marekani Dr. Anthony Fauci amesema kwamba angependa kuisoma ripoti hiyo kabla ya kuamua juu ya uhalali wake. Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ameipokea ripoti hiyo.

"Tutaisoma ripoti na kuijadili, kutathmini maudhui yake na kuchukua hata na nchi wanachama. Lakini kama nilivyosema, dhana  zote ziko mezani na kunahitajika utafiti zaidi na zaidi kwa kile nilichokiona hadi sasa."

Mwaka uliopita uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Associated Press ulibaini kwamba serikali ya China ilikuwa ikidhibiti vikali tafiti zote zinazohusiana na chanzo cha virusi hivyo. Ripoti hiyo imebainisha sababu kadhaa zinazoweza kuwa zimechangia janga hilo, lakini inaondoa uwezekano wa kwamba virusi vilianzia maabara.

Inaongeza kuwa ajali za namna hiyo huwa nadra kutokea, na kwamba maabara za mjini Wuhan zinaendeshwa vyema na hakuna rekodi ya virusi vinavyokaribiana na virusi va corona katika maabara yoyote mjini humo kabla ya Desemba mwaka 2019.

Ripoti hiyo kwa kiasi kikubwa inategemea ziara iliyofanywa na timu ya wataalamu wa kimataifa mjini Wuhan. Katika rasimu ambayo shirika la habari la Associated Press imeiona, watafiti wameorodhesha nadharia nne za uwezekano wa chanzo cha janga la virusi vya corona.

Sababu kuu inatajwa kuwa kuna uwezekano maambukizi yalitoka kwa Popo kwenda kwa binadamu kupitia mnyama mwingine. Popo wanafahamika kubeba virusi vya corona. Ripoti hiyo haijahitimisha ikiwa mlipuko huo ulianzia mjini Wuhan katika soko la vyakula vya baharini lakini soko hilo lilikuwa chanzo cha awali kwasababu ya kuuzwa wanyama wasio wa kawaida, na wengi walihoji pengine wanyama hao ndio walioleta virusi vya corona katika mji huo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...