Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakitia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetia saini mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi 12 ukigharimu Jumla ya shilingi Bilioni 24.4.
Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde na kushuhudiwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga na Singida.
Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui,bwana Murali Mohan.
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema mradi huo unaotarajiwa kutatua kero ya maji katika Miji ya Tinde na Shelui unatekelezwa kwa fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia Exim Bank India.
"Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika mji wa Tyeme kata ya Shelui,kulaza bomba kuu (Transmission main) lenye ukubwa kati ya milimita 400 na 300 kutoka bomba kuu kijiji cha Chembeli hadi Tinde lenye urefu wa kilomita 20.93 na bomba la ukubwa wa milimita 50 kwenye tanki la Didia lenye urefu wa kilomita 1.5",amesema Mhandisi Sanga.
"Shughuli nyingine ni kulaza bomba kuu lenye ukubwa wa kati ya milimita 350 na 200 kutoka bomba kuu linalokwenda Igunga katika kijiji cha Ipumbulya hadi Mgeta, Shelui lenye urefu wa kilomita 70.5,kujenga matanki ya kuhifadhia maji,ukaratabati wa matanki na kujenga vituo vya kuchotea maji",amesema.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji , Jumaa Aweso amesema ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe alilotoa Januari 29,2021 alipopita Tinde na Shelui ambapo alitaka wananchi wa maeneo hayo wapewe huduma ya Maji kutoka Ziwa Victoria.
"Hili ni Jambo kubwa sana na tunamshukuru Mhe. Rais Magufuli. Nimuombe Mkandarasi anayejenga mradi huu kuhakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia mkataba wa mradi na kuhakikisha anamaliza ndani ya miezi 12. Niwaambie tu kuwa hatutaongeza muda",amesema Aweso.
"Mkandarasi hakikisha unamaliza ujenzi kwa wakati kwa kuzingatia mkataba na fedha zitumike kama ilivyopangwa na ikiwezekana chenji ibaki",ameongeza.
Aidha amesema hatamvumilia mtu yeyote atakayethubutu kuhujumu mradi huo akiwataka wananchi kushirikiana na mkandarasi
"Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwepo, Msichezee huu mradi, ukishiba chezea kitambi chako au kidevu chako. Mimi ni Waziri Kijana atakayezingua tutazinguana. Ninachotaka wananchi wapate maji safi na salama kwa gharama nafuu", amesisitiza Aweso.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko alimuomba Waziri wa Maji kuingiza kwenye bajeti za mradi kata za Nsalala, Usule na Bukene kwani zimerukwa katika mradi huo ambapo Waziri Aweso alisema kata ya Nsalala pia itanufaika katika mradi huo wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tinde na Kiomboi.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuzipongeza mamlaka za maji SHUWASA na KASHWASA kwa kazi nzuri wanazofanya katika huduma za maji kwenye wilaya ya Shinyanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Ruhahula amesema mradi huo wa maji utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ya maji katika mji wa Shelui.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amewataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo wa maji na kuhakikisha wanashiriki katika ujenzi wa mradi ili kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kutatua changamoto ya maji katika mji wa Tinde akiomba pia kata zilizosahaulika ziingizwe kwenye mradi na kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kata ya Mwakitolyo.
Nao wananchi wa Tinde akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal wamesema kukamilika kwa mradi wa maji katika mji wa Tinde kutachochea maendeleo ya Tinde kwani yalisimama kutokana na changamoto ya maji.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakitia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Kiomboi imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Utiaji saini ukiendelea
utiaji saini ukiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakionesha nyaraka baada ya kutia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui, bwana Murali Mohan wakionesha mikataba baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakifuatilia Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Dk. Christina Mnzava akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mhe. Albert Msovela akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Ruhahula akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Kulia ni Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal akiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum (katikati mwenye suti) akicheza ngoma ya Mabulo ya Jeshi kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Awali Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiwasalimia wakazi wa Tinde kushuhudia Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso baada ya kufanyika kwa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) baada ya kufanyika kwa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog