Na Timothy Itembe Mara.
Shule za msingi 8 ikiwemo ya sekondari moja Mbogi za halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara kunufaika na mifuko ya sementi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya makau wa Rais muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waita.
Akikabidhi mifuko hiyo katika shule mbalimbali kwa nyakati tofauti Waitara alisema kuwa kufanya hivyo ni kuhakikisha shule zinajengwa na kukamilika ili kuondolea wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifuata masomo.
"Shule zinapokuwa karibu zinasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakutembea kufuata masomo shule za mbali ikiwemo kupunguza mimba mashuleni kwa watoto wa kike"alisema Waitara.
Waitara aliongeza kusema kuwa kipindi cha uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli serikali imedhamiria kuwafikishia wananchi huduma karibu na kuwaondolea adha za mda mrefu kama vileAfya,Elimu,Maji na miundombinu ya barabara.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini,Simion Kiles aliwatupia lawama viongozi waliokuwa wakiuongoza halmashaurri hiyo kwa maana ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kuwa hawakufanya maendeleo pindi waliposhika halmashauri na kuiongoza.
Kiles aliongeza kusema madiwani pamoja na Mbunge wa Tarime vijijini wanapata wakati mgumu wakiulizwa mswala ya miradi iliyokwama kutekelezeka na wananchi kuendelea kuteseka pindi wapaokuwa wanahitaji huduma.
Akitoa mfano mbele ya Mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri na mkurugenzi Apoll Tindwa alisema kuwa kipindi kilichopita halmashauri ilikuwa inaongozwa na CHADEMA lakini miradi mingi imekwama kutekelezeka na wananchi wanaendelea kuteseka na kulaumu viongozi kama vile shule ya Magoto ambayo amechangia ujenzi wa darasa moja kwa nguvu zake mwenyewe.
Kwa upande wake diwani viti maalumu Tarafa Inchage,Rhobi Mwita Nyaihita alisema kuwa Mbunge kutoa mifuko ndani ya shule ya msingi Kihero iliyopo kata ya Nyarero kutasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo taklibani kilomita tano wakifuata masomo shule ya msingi Nyarero.
Nyaihita alitumia nafasi hiyo kushukuru serikali ya awamu ya tano na kuwataka wanajamii kwa ujumla kuunga juhudi za maendeleo serikali bila kutumia nguvu.
Akipokea mifuko na kukabidhi kwa shule husika mkuu wa wilaya Tarime Mtemi Msafiri alisema kuwa serikali imedhamiria kupunguza changamoto zilizopo kwa wananchi na milango iko wazi kwa yeyoye mwenye shida kufika Ofisini kwake ili kutekelezewa.
Msafiri aliongezakusema wananchi kwa ujumla wake wanatakiwa kuunga juhudi za maendeleo ndani ya maeneo yao bila kusukumwa na kuwa Chama cha mapinduzi kimejipanga kuoindoa kero kwa wananchi.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Kihero iliyopo kata ya Nyarero iliyopata mifuku ya sementi 60,Shule ya sekondari Mbogi mifuko 40,shule ya msingi kimusi mifuko 60 na Nyamiri shule ya msingi mifuko 60 nyingine ni shule ya msingi Iteremia mifuko 80,shule ya msingi Kewerumbe mifuko 80 na shule ya msingi Keisaka mifuko 40