Saturday, February 13, 2021

Harmonize na Kajala sio siri tena, waenda Zanzibar kusheherekea siku ya wapendano

Sio siri tena kwani kila kitu kipo wazi kwamba CEO wa lebo ya Konde Gang Harmonize, na msanii wa filamu Kajala Masanja wapo kwenye mahusiano ambapo awali walikuwa wanaficha ficha sana.

Wawili hao wameonekana kuelekea visiwani Zanzibar kusheherekea siku ya wapendano 'Valentine Day' ambapo kupitia Insta Stori ya Harmonize ameonesha kumfanyia 'surprise' Kajala kwa kumpeleka ufukweni usiku kula chakula cha jioni.

Aidha kupitia post ambazo ameshea Harmonize akiwa na Kajala kwenye ukurasa wake wa Instagram amendika kuwa "Karibu kwenye United State Of Konde Gang" Konde Biden na Kajala Kamala, naahidi kuwa kwa ajili".

Ikumbukwe Kajala Masanja ana mtoto mmoja wa kike 'Paulah Kajala' aliyempata na mzazi mwenzie Producer P Funk Majani, pia Harmonize naye ana mtoto mmoja wa kike aliyempata na mzazi mwenza Official Shantel.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...