Saturday, February 13, 2021

ASASI YA INSPIRATIONAL WOMEN GROUP YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA KIGOMA


Viongozi wa Asasi ya Inspirational Women Group pamoja na ofisa elimu taaluma sekondari wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakitoa msaada wa taulo za kike kwa uongozi na wanafunzi wa Buhanda sekondari iliyopo manispaa ya Kigoma Ujiji.
Wanafunzi wa shule ya sekondari za Buhanda na Buteko katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wakifurahia taulo zao za kike walizokabidhiwa na asasi ya Inspirational women Group
Ofisa Elimu taaluma sekondari wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Fredrik Edson akiongea na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Buteko wakati wa halfa ya ugawaji wa taulo za kike shuleni hapo
Ofisa Elimu taaluma sekondari wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Fredrik Edson akiongea na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Buteko wakati wa halfa ya ugawaji wa taulo za kike shuleni hapo
Mwenyekiti wa Asasi ya Inspirational Womem Group Aisha John akitoa mada juu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa Buteko sekondari(hawapo pichani)
Mwenyekiti wa Asasi ya Inspirational Womem Group Aisha John akitoa mada juu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa Buteko sekondari
**

Na Editha Karlo,Kigoma
ASASI ya Kijamii ya Inspirational Women Group wametoa msaada wa taulo za kike 600 kwa watoto wa kike wa shule za sekondari za Buteko na Buhanda zilizopo Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa wanafunzi zaidi ya 450 watanufaika na msaada huo.

Akitoa mada juu ya hedhi salama kwa mtoto wa kike Mwenyekiti wa Women Inspirational Aisha John kabla ya kugawa taulo hizo alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani muda wote na aweze pia kusoma kwa utulivu na kujiamini.

Aisha Alisema suala la hedhi  kwa mtoto wa kike ni suala la kawaida na si jambo la aibu au laana bali ni hatua za ukuaji na kufanya kizazi kijacho kiwe salama.

"Unapokuwa mwanamke na unaingia hedhi jivunie sana usione hili ni jambo la aibu au laana,hapo unakuwa na uhakika wa kuwa unaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto hivyo kuendeleza kizazi",alisema Mwenyekiti huyo.

Aliwataka pia wanafunzi hao wakike wanapoingia kwenye hedhi kuzingatia usafi wakati  na baada ya kuzitumia taulo hizo.

Aliongeza kwa kampeni hiyo ya kuhamasisha hedhi salama kwa mtoto wa kike ni endelevu ambapo wamechagua shule za sekondari za Buteko,Buhanda na Wakulima kuanza nazo katika kampeni hiyo.

Naye Ofisa Elimu taaluma sekondari wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Fredrik Edson akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi taulo hizo  kwa wanafunzi wa sekondari ya Buteko na Buhanda alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani na huru muda wote hii itamfanya aweze kuhudhuria vipindi vya masomo vyote shuleni.

Alisema watoto wakike wanapokuwa kwenye hedhi wanatakiwa wasijisikie wanyonge kwa kukosa taulo za kike na kushindwa kuhudhuria vipindi vya masomo yao kikamilifu.

Walimu wa shule ya sekondari wa Buteko waliwashukuru Inspiration Womem Group pamoja na wadau wote walioshiriki kuwasaidia watoto wa kike shuleni hapo kwa  kuwapatia taulo za kike kwani kutawafanya wasome kwa kujiamini na kutopoteza kipindi hata kimoja wakati wanapokuwa kwenye hedhi.

"Kwa kweli mmefanya jambo zuri sana tunaomba hili jambo liwe endelevu kwani hii inawasaidia wanafunzi wa kike kuwa na uhakika wa masomo na kuacha tabia ya kuacha kuja shule wanapo kuwa kwenye hedhi",alisema mmoja wa walimu.

Naye Imaculate Emanuel, mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Buhanda amesema msaada huo wa taulo za kike kwao umekuja wakati muafaka na ni wa maana sana kwao kwani mahudhurio ya shule sasa yatakuwa mazuri kwa wanafunzi wa kike.

Alisema watoto wa kike wamekuwa wanakutana na changamoto wanapi kuwa kwenye hedhi hulazimu kurudi nyumbani huku masomo yanakuwa yakiwapita.

"Tunawashukuru kwa msaada huu wa taulo za kike baadhi tulikuwa tunashindwa kuzinunua tunapokuwa kwenye hedhi kwasababu ya kushindwa kumudu gharama na taulo hizi na tunajisikia wanyonge tunapoingia kwenye hedhi na kukosa taulo za kike ila sasa hivi hali itakuwa tofauti tumepewa elimu juu ya hedhi salama na msaada huu wa taulo tutajiamini na kuhudhuria vipindi vyote kila mwezi", alisema
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...