Sunday, January 3, 2021

VIDEO: Naibu Waziri awacharaza bakora watu wanaowaendesha walemavu kuomba pesa


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amekemea vikali vitendo vya udhalilishaji Watu wenye Ulemavu ikiwemo suala watu ambao wamekuwa wakitumia kundi hilo kujinufaisha.

Hayo yameelezwa wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika maeneo mbalimbali ambayo wanahifadhiwa Watu Wenye Ulemavu katika Mtaa wa Tandale, Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri alieleza kuwa kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji wa watu wenye ulemavu ambavyo vimekuwa vikiendelea katika jamii na vitendo hivyo vinapelekea ukiukwaji kwa haki zao.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...