Sunday, January 3, 2021

Wananchi Kiteto waungana na wadau kukarabati bwawa la maji


Na John Walter-Kiteto.

Wananchi wa Kijiiji cha Olpopong'i, wilayani Kiteto mkoani Manyara, wameungana na Chama cha msalaba mwekundu Tanzania, kukarabati bwawa lao la maji ambalo ni chanzo pekee kinachotumika kupata maji tena wakishirikiana na mifugo.

Hatua hiyo imefuatia wananchi hao kutokuwa na chanzo kinginge cha maji, hali iliyofanya washindwe kupata maendelea mengine kwa kutumia muda mwingi kusaka maji kuliko kufanya shughuli zingine za maendeleo, ndoo moja inauzwa 500.


"Maji tunayotumia sio safi na salama...tunashirikiana na mifugo, na baadhi ya wenzetu wanaoga ndani ya bwawa, ni Mungu tu ndio anatusaidia tusipatwe na maradhi kama vile kuhara na hata kipindupindu" alisema Magdalena Saitoti.

Kwa upande wake, Haji Juma Makorokoro mmoja wa mwananchi hao alisema, Chama cha msalaba mwekundu Tanzania, kimekuwa msaada mkubwa kwao kwani kwa sasa watakuwa wanapata maji safi yatatumika kwa utaratibu maalumu.

Alisema utaratibu huu utalinda bwawa hilo lisikauke mapema na pia maji hayo yatakuwa safi tofauti na awali ambapo mifugo ilikunywa humo humo, mtu alikuwa akitaka poa kuoga aliogea humo humo..hatari sana.

Meneja wa mradi wa usalama wa Chakula Kiteto wa Chama cha msalama mwekundu Tanzania, Haruni Mvungi, akizungumzia namna wanavyoshiriki kukarabati bwawa hilo alisema, wako katika eneo lao la mradi ambalo ni vijiji vinne Orpopong'i, Ndaleta, Ndedo na Makame.

Alisema baada ya wananchi kueleza ukubwa wa tatizo la maji, Chama cha msalaba mwekundu Tanzania ambacho nia yake pamoja na mambo mengine ni kupunguza ama kuondoa madhara kwa wananchi kimeungana na wananchi hao kukarabati bwawa hilo.

"Ukarabati tunaofanya ni kuondoa matope na uchafu ulioingia ndani ya bwawa, kazi hii inafanywa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na wataalamu toka Serikalini, ambao ni Wakala wa maji mjini na vijijini Ruwasa"

Alisema katika kazi hiyo wananchi wanalipwa ujira kidogo ili waweze kuendesha maisha yao na pia wanapata ujuzi wa namna ya kukarabari bwawa wenyewe ii siku likiharibika iwe rahisi kukarabati wenyewe.

Wakala wa maji mjini na vijijini Ruwasa, Mhandisi Stephano Mbaruku alikiri wananchi hao kukabiliwa na tatizo la maji akisema Serikali imejipanga kuhakikisha wanapata maji safi na salama.

Awali kulikuwa na mashine ya maji, kuna baadhi ya wananchi walihujumu, sasa tumewakamata watalipa, hivyo tutanunua mashine nyingine haraka ili waendelee kunufaika kupata maji safi alisema Mbaruku.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...