Thursday, December 3, 2020

MGODI WA STAMIGOLD BIHARAMULO WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA... YAOMBA UMEME

Kampuni ya Stamigold ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia mgodi wake wa Stamigold Biharamulo (Stamigold Biharamulo Mine - SBM) uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera imeshiriki katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika eneo la Butulwa Old Shinyanga Mkoani Shinyanga.

Kilele cha Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini yaliyoongozwa na kauli mbiu ya 'Biashara na madini ni chachu ya maendeleo Shinyanga' kimefanyika Disemba 1,2020 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula. 

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, alisema mgodi huo unakabiliwa na gharama kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu hivyo kuiomba serikali iwapunguzie gharama kwa kuwaunganishia huduma ya umeme kutokana na kutumia genereta na mafuta ya dizeli.

"Tangu mgodi huu uwe chini ya Serikali mwaka (2014), na kuanza uzalishaji rasmi 2017, umekuwa ukiingia kwenye gharama kubwa ya uzalishaji dhahabu, kutokana na kutumia Jenereta na mafuta ya Diesel. Tunaiomba Serikali ituunganishie huduma ya umeme kwenye mgodi huu, ili tupunguze gharama kubwa ya uzalishaji", alisema Mhandisi Shamika.

"Kutokana na kutumia Jenereta na mafuta ya Diesel tunalazimika kutumia Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwezi na endapo tutapata huduma ya umeme gharama itapungua na tutatumia shilingi Milioni 300",aliongeza Mhandisi Shamika.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akiwa kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, aliupongeza mgodi huo kwa kufufuka tena na kuanza uzalishaji wa madini.
Kulia ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (katikati aliyevaa miwani) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga Disemba 1,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (wa pili kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga
Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (wa pili kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu
Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020.
Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...