Wednesday, December 2, 2020

ADA TADEA yatoa maamuzi kuhusu uchaguzi ujao


Chama cha ADA TADEA ambacho ni moja ya chama cha upinzani kilichoshiriki kwenye uchaguzi wa 2020  kimesema kipo kwenye wakati wa kufanya tathimini za uchaguzi ili kujipanga upya kwa uchaguzi ujao.


Akizungumza na EATV Digital Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA John Paul Shibuda amesema kuwa chama hicho kiko katika wakati wa kufanya tathmini juu ya uchaguzi ambazo zitasaidia kukijenga chama hicho na kukisaidia kujipanga upya katika majimbo yote.


"Bado tupo kwenye tathmini ya masuala ya uchaguzi wa maeneo yote bara na visiwani , ambapo tunataka kujua hapa kulikuwa na nini, madhaifu, mapungufu, nguvu tulizokuwa nazo, uchaguzi huu una maneno mengi" amesema Shibuda 


"Vyama vilivyoshiriki uchaguzi vina maoni yake na mtazamo wake huwezi kusema mpango wetu wa uchaguzi ujao ni hivi wakati ujakamilisha tathmini ya mambo mabalimbali ujue mapungufu yenu na mazuri yenu na hii si kwa chama kimoja lazima uangalie na mpinzani wako aliyeshiriki alikuwa na nguvu gani na mapungufu gani, ni lazima ujue chama pinzani kilikuwa na mapungufu gani ndio unatengeneza nguvu zako za ushindani" amesema Shibuda

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...