Saturday, December 26, 2020

Maadhimisho ya kiongozi Jinnah Pakistan


Mwanzilishi wa Pakistan na Kaid-i Azam wa taifa (Baba Kiongozi wa Taifa) Mohammed Ali Jinnah anaenziwa katika maadhimisho ya miaka 144 tangu kuzaliwa kwake.

Kila tarehe 25 Desemba, kumekuwa kukiandaliwa sherehe mbalimbali kote nchini za maadhimisho ya Jinnah aliyezaliwa mwaka 1876 mjini Karachi, ambapo hukumbukwa kwa simulizi za mapambano ya kisiasa, uongozi na maisha yake binafsi.

Pamoja na ushiriki wa maafisa wa serikali na raia, Kurani tukufu pia husomwa katika kaburi la Jinnah linaloitwa "Mezar-ı Kaid" lililoko mjini Karachi.

Jumba la Wazir, ambalo Jinnah alizaliwa huko Karachi, lilibadilishwa kuwa kaburi la kitaifa na jumba la kumbukumbu, na linatembelewa na raia.

Kutokana na janga la virusi vya corona (Covid-19), semina, mikutano na maonyesho ya kusimulia maisha ya Jinnah mwaka huu yalifanyika kwenye majukwaa ya mitandao. Vituo vya televisheni pia viliandaa vipindi maalum kuhusu mapambano ya Jinnah kwa ajili ya Pakistan.

Wanasiasa wengi, haswa Rais wa nchi Arif Alwi na Waziri Mkuu Imran Khan, walichapisha ujumbe kuhusu maadhimisho ya miaka 144 ya siku ya kuzaliwa kwa Jinnah.

Jinnah alikufa mjini Karachi mnamo Septemba 11, 1948 kutokana na maradhi ya kifua kikuu na matatizo mengine ya kiafya.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...