Wanamazingira, maafisa wa serikali na maafisa wa eneo nchini Kenya wameungana kuokoa twiga wanane waliokuwa wamekwama katika maeneo ya kisiwani.
Walijenga mashua za kusaidia wanyama kuvuka.
Na hadi kufikia sasa, wawili wamefanikiwa kupita salama.
Kwa mujibu wa David O'Connor wa Shirika la Save Giraffes, ameelezea BBC Newsday, kuwa juhudi hizo zilianza miaka mitatu iliyopita pale maji ya Ziwa Baringo yalipoanza kuongezeka.