Wawakilishi wa Uingereza na Umoja wa Ulaya kwa mara nyingine tena hapo jana wameshindwa kufikia makubaliano katika mazungumzo ya kusaka mkataba wa kibiashara. Badala yake wamewakabidhi kibarua hicho
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.
Viongozi hao watawasiliana kwa njia ya simu hii leo, baada ya wajumbe wao Michel Barnier na David Frost kufanya mikutano ya mchana na usiku kwa wiki nzima bila mafanikio.
Uingereza inatarajiwa kumaliza kipindi cha mpito cha majadiliano mnamo Desemba 31, baada ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Mpango wa kibiashara unahitajika ili kuepusha usumbufu kwa chumi za pande zote mbili. Hasa Uingereza ambayo tayari uchumi wake umeanguka kutokana na janga la virusi vya corona.
Source