Maandamano dhidi ya ubakaji yamekuwa yakifanyika kote nchini Pakistan katika miezi ya hivi karibuni baada ya ubakaji mbaya uliotokea mwezi Septemba.
Kulingana na sheria hii , serikali itaweka sajiri ya watu wanaopatikana na makosa ya ubakaji, kulinda utambulisho wa waathiriwa na matumizi ya kemikali kuwahasi baadhi ya wabakaji.
Kulingana na sheria hii, kesi za ubakaji zitaharakishwa. Mahakama zinatarajiwa kukamilisha kesi ya ubakaji ndani ya kipindi cha miezi minne.
Serikali imesaini sheria mpya dhidi ya ubakaji baada ya malalamiko mengi ya watu dhidi ya unyanyasaji huo wa kingono baada ya wanaume kadhaa kumbaka mwanamke mmoja nje ya jiji la Lahore.
Walimbaka mwanamke huyo kando ya barabara inayoelekea katika jiji hilo mbele ya watoto wake wawili. Mkuu wa polisi alisema kuwa muathiriwa kwa upande mmoja alikuwa na makosa.
Wanawake na watoto wa kike wamekuwa wakibakwa na kuuawa nchini Pakistan.
Kauli yake pamoja na unyanyasaji huo wa kinyama viliwakasirisha watu nchini humo ambao walisema kuwa amegeuza ukatili huo kuwa kitu kidogo. Maandamano makubwa yamekuwa yakiendelea kuilazimisha serikali kuchukua hatua dhidi ya ubakaji.
Waziri Mkuu Imran Khan na baraza lake la mawaziri waliidhinisha sheria hiyo na Rais Arif Alvi akisaini kuwa sheria Jumanne
Serikali ilipewa siku 120 na umma kuwa imeidhinisha sheria hiyo na kupitishwa na bunge.
CHANZO - BBC SWAHILI