Thursday, December 31, 2020

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI PATROBAS KATAMBI AFUNGA MWAKA 2020 KWA ZIARA BABU KUBWA....AMWAGA MILIONI 23


Naibu Waziri Katambi akishiriki kubeba mchanga kwa ajili ya kuujaza kwenye msingi unaojengwa chumba kimoja cha darasa katika shule ya Msingi Negezi

Na Damian Masyenene –Shinyanga 
NAIBU Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM), leo amefanya ziara ya kikazi jimboni humo kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha shule zitakapofunguliwa Januari mwakani wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na wanaoanza darasa la kwanza waende shule. 

Katambi amefanya ziara hiyo katika kata nane za jimbo hilo ambazo ni Chamagua, Ndembezi, Ngokolo, Ibinzamata, Ndala, Kitangiri, Masekelo na Mwasele, huku akiambatana na Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila na Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Geofrey Mwangulumbi pamoja na watumishi wa idara ya elimu na madiwani. 

Shule za msingi na sekondari zilizokaguliwa na Katambi katika ziara hiyo ni shule ya msingi Ushirika, Ndala A, Ibinzamata, Neghezi na Msufini, huku akizitembelea shule za sekondari za Mazinge, Ngokolo, Town, Mwasele, Busulwa, Ibinzamata, Masekelo na Ndala. 

Naibu Waziri Katambi amechangia jumla ya Sh Milioni 23 kwa ajili ya Kukamilisha ujenzi wa vyumba 24 vya madarasa na ofisi tatu za walimu katika shule 13 alizozitembelea kwenye kata nane za jimbo hilo. 

Akizungumza katika Ziara hiyo, Katambi ameeleza kuwa ujio wake ni msisitizo na utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaka ujenzi wa vyumba vya madarasa umalizwe ifikapo Februari 28, mwakani na kuhakikisha kwamba hakuna mwanafunzi anakosa nafasi ya kwenda shule kwa sababu ya upungufu wa madarasa. 

Naibu Waziri huyo amewashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha wa kuchangia nguvu katika ujenzi wa vyumba hivyo wakisaidia kwa kuchanga fedha, kuchimba misingi, kusomba kokoto na maji pamoja na kusaidia kazi za ufundi kwa gharama nafuu, huku akibainisha kuwa fedha alizoahidi zitakabidhiwa kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa. 

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila, ambaye alichangia Sh 100,000/= na mifuko mitano ya saruji katika shule ya sekondari Mazinge, amesema kuwa halmashauri imewaelekeza wataalam wajipange ujenzi huo uwe mpango endelevu utakaosaidia kumaliza changamoto ya upungufu wa madarasa. 

"Kwa sasa kila shule inafanya harakati za kumaliza ujenzi wa madarasa yanayohitajika kwa uharaka ili watoto waweze kuripoti shuleni kwa muda unaohitajika. Tulivyojipanga baada ya kumaliza hili jambo la haraka, tutaendelea kujenga madarasa ili yawepo muda wote yatakapohitajika," amebainisha. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi amesema kuwa halmashauri ilitoa walau Sh Milioni 5 kwa baadhi ya shule zenye uhitaji mkubwa na zingine Sh Milioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, huku akiweka wazi kuwa kwa sasa wanao upungufu wa vyumba 100 vya madarasa vikiwemo 34 kwa shule za sekondari na 66 kwa Shule za msingi. 

Ambapo jumla ya Sh Bilioni 2 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo, hivyo akaomba ushirikiano kwa wadau wote na kwamba Kamati ya fedha ya manispaa hiyo ikiongozwa na Mstahiki Meya ilibuni mikakati kadhaa ikiwemo kuchangisha wananchi na wadau wengine wa maendeleo. 

Vile vile, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abubakari Gulam ameahidi kutoa mifuko 10 ya Saruji itakayokabidhiwa wiki ijayo katika shule ya Sekondari Ngokolo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, aahadi hiyo imetolewa baada ya Kaimu Mtendaji wa Kata ya Ngokolo, Salum Soud kuelezea kuwa wanao upungufu wa vyumba 8 vya madarasa, vikiwemo vya haraka vinne, ambapo tayari wameanza na vitatu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA
Naibu Waziri Patrobasi Katambi (kushoto aliyekaa) akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika katika shule ya msingi Ushirika iliyopo kata ya Chamagua kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa. Picha zote na Damian Masyenene.
Mheshimiwa Katambi pamoja na viongozi wengine wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Ushirika
Afisa Elimu Kata ya Chamagua, Fransisca Msindu akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika kata yake
Mh. Katambi akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Ngokolo
Afisa Elimu Kata ya Mwawaza, Jacob Sallu akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kata hiyo
Naibu Waziri Katambi akishiriki kubeba mchanga kwa ajili ya kuujaza kwenye msingi unaojengwa chumba kimoja cha darasa katika shule ya Msingi Negezi
Naibu Waziri wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (aliyeshika koleo), akishiriki katika kuondoa udongo kwenye msingi wa chumba kimoja cha darasa unaojengwa katika shule ya msingi Msufini iliyopo Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga, leo wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa madarasa katika jimbo lake
Naibu Waziri Katambi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam wakishiriki kujaza udongo kwenye msingi unaojengwa kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Town
Naibu Waziri Katambi (aliyebeba tofali) akimsaidia fundi kuweka tofali kwenye msingi unaojengwa kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Masekelo 
Naibu Waziri Katambi akishiriki katika kuchimba msingi kwenye shule ya Msingi Msufini
Naibu Waziri Katambi akichota mchanga na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi akitega ndoo kwa ajili ya kuweka mchanga huo wakati wa ziara yao ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Town
Katambi (aliyesimama kushoto) akifurahia jambo na mafundi wanaojenga madarasa katika shule ya Sekondari Mwasele, baada ya kufika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
Naibu Waziri Katambi akikaribishwa na baadhi ya wanachama wa CCM katika Kata ya Ndembezi alipowasili katika shule ya Sekondari Mazinge kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa
Mheshimiwa Katambi akimkabidhi fundi ndoo yenye mchanga kwa ajili ya kuumwaga katika msingi unaojengwa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Town
Naibu Waziri Katambi akikaribishwa na baadhi ya wanachama wa CCM alipowasili katika shule ya sekondari Ibinzamata
Mheshimiwa Katambi akisalimiana na baadhi ya akina mama waliofika kwenye ziara yake katika shule ya msingi Msufini
Naibu Waziri Katambi akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ibinzamata
Katambi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinzamata
Jengo lenye chumba kimoja cha darasa linalojengwa katika shule ya sekondari Ngokolo
Jengo la chumba kimoja cha darasa na ofisi ya mwalimu mkuu linalojengwa katika shule ya sekondari Busulwa iliyopo Kata ya Kitangiri
Jengo la vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu ambalo limefikia katika hatua ya umaliziaji linalojengwa katika shule ya msingi Ibinzamata 
Mkuu wa shule ya sekondari Ndala, Iman Chambulilo (kulia) akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo
Mh. Katambi akitoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi baada ya kufanya ukaguzi katika shule ya sekondari Ngokolo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Patrobas Katambi wakati wa ziara yake katika shule ya msingi Ndala A
Mkuu wa shule ya msingi Town, Jason Rwegasira akisoma taarifa ya utekelezajiwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ndala A,Rajabu Khamsini akisoma taarifa 
Mafundi wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msufini
Mafundi wakiendelea na kazi ya kuchimba msingi katika shule ya msingi Neghezi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila akiwa amebeba ndoo yenye mchanga kwa ajili ya kuujaza katika msingi wa chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi Neghezi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi (aliyeshika karatasi) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Patrobas Katambi wakati wa ziara yake katika shule ya sekondari Mazinge
Msingi wenye vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mazinge
Msingi wenye vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mwasele
Mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa msingi katika shule ya sekondari Ngokolo
Msingi utakaojengwa chumba kimoja cha darasa katika shule ya sekondari Ndala
Msingi utakaojengwa darasa lenye vyumba viwili katika shule ya msingi Ushirika
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam akiwa amebeba ndoo yenye mchanga kwa ajili ya kuujaza kwenye msingi unaojengwa chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi Neghezi
Mkuu wa shule ya sekondari Masekelo, Stephen Mihambo akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo
Naibu Waziri Katambi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwasele, Suzana Manoni (kulia) wakati wa ziara yake shuleni hapo
Katambi akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinzamata
Ukaguzi ukiendelea
Ukaguzi ukiendelea

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG


Waziri Gwajima aipongeza hospitali ya Muhimbili kwa kuwa na huduma za ubingwawa hali ya juu




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwa na huduma za ubingwa wa hali ya juu ambao haupatikani katika nchi nyingi za kiafrika.



Waziri Gwajima ametoa pongezi hizo leo wakati alipofanya ziara katika Hospitali hiyo ili kuona hali ya utoaji wa huduma hususan katika vitengo mbalimbali kama kitengo cha huduma za dharura, wodi ya wagonjwa mahututi, wodi za watoto n.k.
"Nimeamua kuja hapa Muhimbili kwanza kuona hali ya utoaji wa huduma, kuona mafanikio na changamoto lakini pia kuona mwelekeo wao kwa ujumla. Kifupi napenda kutambua mchango wao mkubwa katika kuboresha huduma za afya nchini na zaidi huduma za ubingwa na ubingwa wa hali ya juu". Amesema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema katika kipindi cha miaka mitano Hospitali ya Muhimbili imechangia kwa kiasi kikubwa kuokoa fedha za Serikali kwa kupeleka wagonjwa wa rufaa nje ya nchi kutokana na huduma nyingi za kibingwa kuanza kupatikana Hospitalini hapo.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema Hospitali hiyo ya Taifa imejipanga vyema katika kipindi cha miaka mitano ijayo ambapo kutaanzishwa huduma ya kupandikiza uroto wa mifupa (Bone marrow transplant) huku wataalamu wa kufanya kazi hiyo wakiwa tayari wameshafika na baadhi ya vifaa vikiwa tayari vimefungwa na hivi sasa kinasubiriwa kifaa kimoja kifike ili huduma hiyo ianze kutolewa kuanzia mwezi Machi mwakani.



Pamoja na kujiridhisha na huduma mbalimbali zinazotolewa katika Hospitali hiyo, Dkt. Gwajima pia ametembelea ujenzi wa jengo litakalotumiwa na wagonjwa binafsi wenye haraka (Fast Track Services) ambalo Serikali imetoa zaidi ya Bilioni nne za kufanikisha ujenzi huo ambao upo katika awamu ya kwanza.
Dkt. Gwajima ameipongeza Hospitali hiyo kwa kuwa na huduma ya kutoa misamaha kwa wagonjwa wasiojiweza lakini amewataka wananchi kufuata taratibu zilizowekwa ili kupata misamaha hiyo kuliko kulalamika. Pia ameendelea kusisitiza wananchi wajiunge na mifuko ya bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa na NHIF ili waondokane na gharama kubwa za matibabu pindi wanapopata changamoto za afya.

Halikadhalika Dkt. Gwajima amewataka watumishi wa afya kutanguliza mbele kutoa huduma kwa wagonjwa kwanza halafu gharama za matibabu zifuate badae, lengo likiwa ni kuzuia vifo vinavyoweza kutokea kwa ucheleweshaji wa kupata matibabu.

Hospitali ya Muhimbili inatoa misamaha ya matibabu takriban Milioni 800 hadi 900 kwa mwezi.

 _

Uchawi Mbeya : MWANAMKE MWENYE UJAUZITO WA MIEZI 9 AJIKUTA HANA MIMBA

Picha ya mwanamke mwenye mimba.

Taharuki imeibuka kwa wakazi wa kitongoji cha Iyula A katika kata Iyula, wilayani Mbozi, baada ya mwanamke mmoja Mariam Mligo (19) anayedaiwa kuwa mjamzito wa miezi tisa, ujauzito wake kupotea katika mazingira tata muda mfupi baada ya kushikwa na uchungu.

Tukio hilo lililozua taharuki kubwa katika Kata ya Iyula, ambapo mama huyo awali alipaswa kujifungua Desemba 25, 2020, na baadaye mama huyo kujikuta hana ujauzito.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Iyula A, Mawazo Mwamlima, amesema kuwa tukio hilo limesababisha taharuki na sintofahamu kwa wakazi wa kitongoji hicho kwa kuwa si tukio la kawaida na kwamba hata mara baada ya kumpeleka hospitali hakuonesha dalili yoyote ya kwamba labda amejifungua.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Mbozi, Dkt. Mponjoli Mwangosi, amethibitisha kumpokea mwanamke huyo katika kituo hicho cha Afya Iyula akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, ambapo uchunguzi wa awali ulionesha kuwa mama huyo hakuwa na ujauzito.

Aidha Dkt. Mponjoli ameongeza kuwa hali hiyo ipo kwenye mambo ya uzazi kwa akina mama na kuna kitu kinaitwa mimba isiyo halisia 'Pseudocyesis Pregnance", hali hiyo huwaingiza watu wengi kwenye migogoro ya ndoa na kuibua taharuki wakisema kuna mambo ya kishirikina, hali hii ambayo hutokana na magonjwa ya wanawake.

Chanzo- EATV

Simba SC namba moja duniani, yaiwacha mbali Tottenham, Inter, Sevilla na timu nyingine



Mabingwa wa Nchi Simba SC imetajwa kama Klabu namba moja duniani ambayo ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Istagram kukua kwa kasi na kuzipiku Tottenham, Sevilla, Inter na timu nyingine.



Takwimu hizo zimetolewa na mtandao wa Transfer Marketing unaojihusisha na maswala ya mchezo wa soka duniani.

Kwa mujibu wa transfermarket, Simba SC imeshika nafasi ya kwanza kwa akaunti yake kukuwa kwa kasi zaidi duniani kwa asilimia +89, ikiwa na wafuasi Mil 1.9 ikifuatiwa na Trasfermerket nafasi ya pili kwa asilimia +76 wafuasi Mil 3.9 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Leverkusen ikiwa imekuwa kwa asilimia +66 huku wafuasi Mil 1.1

Kwa upande wao Simba wameandikwa ujumbe ufuatao "Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market, Simba Sports Club ndio klabu ambayo imeongoza duniani kwa ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Istagram kukua kwa kasi. Chama kubwa hili weka mbali na watoto." – Simba SC

Oktoba 22/ 2020 Mtandao huu uliwahi kumuandika Mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Mbwana Samatta kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wametembelewa zaidi kwenye mtandao wa Transfer Marketing wakati wa dirisha la usajili wa majira ya Joto.



Kwa mujibu wa transfermarket, Samatta ametinga tatu (3) bora kwenye Orodha hiyo inayoongozwa na mchawi wa soka Lionel Messi nafasi ya pili ikichukuliwa na fundi wa mpira Cristiano Ronaldo huku ya tatu ikienda kwa Mtanzania, Captein Diego, Samatta.

Brexit: Makubaliano mapya ya kibiashara kuanza kutekelezwa baada ya bunge kupiga kura


Makubaliano ya baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya kati ya pande hizo mbili kuanza kutekelezwa Alhamisi 23:00 baada ya kutiwa saini kuwa sheria.

Bunge liliunga mkono makubaliano hayo kwa haraka mno Jumatano, baada ya pande hizo mbili kufikia makubaliano mkesha wa Krismasi.

Uingereza inajiondoa katika soko la pamoja la Umoja wa Ulaya na umoja wa forodha lakini makubaliano hayo yanatamatisha uwezekano wa kodi kwa bidhaa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewashukuru wabunge na kusema: "Hatima ya nchi hii muhimu sasa ipo mikononi mwetu."

Lakini wapinzani wanasema nchi hiyo itakuwa vibaya zaidi hata kuliko ilivyokuwa ikiwa kwenye Umoja wa Ulaya.

Kujiondoa kwa Uingereza kunatokea Januari 31, lakini hadi kufikia sasa Uingereza imeendelea kufuata sheria za biashara za Brussels.

Makubaliano hayo yamefikiwa muda mfupi tu kabla ya siku ya mwisho iliyowekwa kufanya hivyo na kutoa mwongozo mpya wa kibiashara na uhusiano wa kiusalama baada ya pande hizo mbili kutengana.

Hatua hii inawadia miaka minne na nusu tangu Uingereza ilipopiga kura ya kujiondoa Umoja wa Ulaya katika kura ya maamuzi.

DALILI 7 Za Kuonyesha Anakucheat Na Mwingine..!!


Katika mahusiano huwa kuna changamoto tofauti tofauti. Kwa kawaida ni muhali kupata mahusiano ambayo hayana patashuka moja au nyingine. Inajulikana ya kuwa mahusiano huwa kuna migogoro, kutoelewana, kunyamaziana na mbaya zaidi...vita.

Anyway mambo kama haya huwezi kuyazuia kwa sababu wenyewe ndio wanayaita mapenzi. Utaskia mtu akilalamika kuwa amemiss kugombana ama kuteteshana na mpenzi wake, jambo ambalo huwa ni la kawaida.

Ok. tukija katika mada yetu ni kuwa nataka nikuulize maswali yafuatayo. Je hivi karibuni umeona kama mpenzi wako amekuwa mtu tofauti na ilivyo kawaida? Je mpenzi wako imekuwa muda mrefu tangu mfanye mambo yenu ya kawaida ambayo mlikuwa mkifanya? Je unamshuku kama amepata mwingine?

Kama majibu yako ni NDIO basi hili chapisho nimeliandika spesheli kwako na nataka umakinike kwa kusoma dalili zetu tulizoziandika na kama yote yanawiana na dhana yako basi ni wakati wa kumfungukia mpenzi wako na umwambie kweupe kuwa umechoshwa na tabia yake ya 'kutoka nje', na umuulize kama amechoshwa nawe ili ukate minyororo ya kuwa naye ili uwe huru.

Zama nami!

Dalili #7: Muda mwingi anajaribu kujirembua kuoneka vizuri

Kuvalia vizuri kila wakati si jambo baya la kufanya katika mahusiano, mwanzo wapenzi hupenda sana kuhakikisha ya kuwa wanampendeza mwenza wao.

Lakini, ukiona ya kuwa anamakinika zaidi na upande wa kujifanya aonekane mrembo, basi itakuwa anajaribu kumridhisha mtu mwingine kando na wewe. Kama umemgundua kuwa anajaribu kuvalia vizuri wakati anatembelea hizi sehemu basi weka ? katika mawazo yako: Kazini, supermarket, mkahawa, na hata gym!

Makinika: Zile sehemu zake za kawaida anazozienda kama amezijeuza kuwa fashion show itakuwa ni ishara ya kuwa anakucheat.

Dalili #6: Anakuwa msiri na simu yake, pakatalishi yake nk

Kila mtu ana haki ya kuwa na faragha yake. Mwanzo, watu wengi hawapendi faragha yao ishambuliwe na hata wapendwa wao. But ishu itakuja wakati ambapo anakuwa msiri kuhusu vitu vyake zaidi kuliko awali.

Hii inaweza kumaanisha kuwa kunakuwa na migogoro isioisha wakati ambapo umechukua kuangalia simu yake hadi ule wakati anaudhika wakati umeingia kwa chumba chake akiwa anatumia kompyuta yake. Ukiona mtu akianza kuwa msiri zaidi ni kuwa atakuwa anawasiliana na mchumba mwingine ambaye ako naye.

Dalili #5: Anapunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa hadi kukataa asilani

Hata watu waseme nini, kufanya mapenzi ni sehemu muhimu inayohitajika katika mahusiano. Kama hamfanyi mapenzi, utajihisi ya kuwa unabezwa na kukatalika na mpenzi wako.

Wakati umri unaposongea, utagundua ya kuwa kiasi cha mapenzi mnachofanya huwa kinapungua. Hio ni kawaida, lakini kuna hatua nyingine neno 'ni kawaida' linaondolewa.

Kukataliwa katakata kufanya mapenzi ama kutoa visababu inaweza kumaanisha kwa njia rahisi kuwa hajiskii kufanya mapenzi na wewe. Wakati mtu anakucheat, huwa anapoteza ule muungano wa kihisia na wewe na atakuwa hana hamu ya kufanya mapenzi na wewe

Dalili 4: Kuna yule mtu kilinge (mysterious)

Wale watu kilinge ndio unaopaswa kuwaogopa zaidi. Wanaume na wanawake kwa kawaida watakuwa na marafiki wa jinsia ile nyingine, lakini kama utamwona mpenzi wako haachi kuongea kuhusu huyo mtu basi kuna tatizo.

Hata kama nia yake ni nzuri, anaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuwa marafiki. Kama hatakuruhusu ukutane na huyu mtu kilinge ambaye amekuwa akipoteza muda wake mwingi naye, basi kunaweza kuwa na kitu ambacho ni zaidi ya kuchat pekee.

Dalili #3: Anazozana na wewe zaidi ya kawaida

Kukefyakefya na kukufananisha na wengine ni jambo lisilokubalika katika usuhiano. Wakati ambapo hii itatoka kuanzia mzaha hadi kuwa serious, ni ishara ya kuwa anakucheat.

Mara nyingi, mpenzi akikosana na mwenziwe hujaribu kujitenga na majibizano. Lakini ukiona ya kuwa kila wakati anagombana na wewe kwa sababu ya mahusiano yenu basi ni ishara ya kuwa kuna mwingine ambaye anamwonyesha mapenzi ya dhati...na si wewe

Dalili #2: Anakutenga wewe na marafiki zako wa karibu

Wapenzi wawili ambao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu huwa wanagawa marafiki pamoja. Hawa ni wale ambao nyinyi wawili mnawaingiza katika maisha yenu kadri miaka inavyosonga. Wakati umeona kuwa mpenzi wako anapunguza muda wa kuwa na wewe na anachofanya ni kuwatenga watu hawa, kawaida huwa kuna mtu anahusika.

Anaweza kuwa hana moyo wa kukabiliana na marafiki wa karibu na kuwadanganya kuhusu furaha anayopata katika mahusiano yenu. Hii inaweza kutokea baada ya muda mrefu ama akajitenga ghafla.

Dalili #1: Analijeuza neno ''tu'' hadi ''ni'' polepole

Neno ''tu'' katika mahusiano ni takatifu. Huu ni ule wakati ambao mwanaume na mwanamke wamewekeza shina la kuwa pamoja. Wakati mwingi, sana sana wanawake ndio huwa wa kwanza wa kubadilisha neno ''ni'' hadi ''tu'' halafu mwanaume akalizoea.

Hivyo katika mahusiano ukiona mpenzi wako ameanza kurudia kutumia neno ''ni'' itakuwa anajaribu kukutenga katika maisha yake, anajaribu kukufuta katika picha yake.


Mwisho ni kuwa kudanganya katika mahusiano ni swala zito ambalo linaibua hisia nzito, lakini dalili za kucheat zinaweza kutatiza zaidi.

Kukataa kufanya mapenzi ama kujaribu kujirembua inaweza kusababishwa na misongo ama kutojiskia shangwe yeye mwenyewe. Kabla ya kumlaumu kuwa anafanya mabaya, hakikisha ya kuwa kuna ishu inayoendelea, ama inaweza kuwa wewe ndiwe chanzo cha kufanya mahusiano yenu yavunjike

Haji Manara Atoa MPYA "Hivi Nikiondoka SIMBA Namuachia Nani Ukubwa wa Jina Langu Unaniponza?


Mkuu wa Idaya ya Habari na Mawasilino Simba SC, @hajismanara amewajibu baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wamekua wakimtabiria mabaya kuhusu kazi zake ndani ya klabu hiyo.


#Manara ametuma majibu hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kufuatia madai yaliyotolewa na baadhi ya wadau hao wakisema amesimamishwa kazi, huku akitakiwa kutozungumza lolote kuhusu Simba SC.


#Manara ameeleza kuwa, bado yupo Simba SC, na ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida, huku akiwatuliza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


"Please Please Please (Tafadhali) Wanasimba mimi Haji wenu bado nipo nanyi na nitaendelea kuwa msemaji wenu hadi pale riziki yangu itakapokwisha, (Hatatokea mmoja wetu kubaki milele iwe kwa kifo au vinginevyo).


"Waambieni wenye kuandika tetesi za kuondoka kwangu, mimi mtu dhaifu lakini ni mjuzi mno katika mambo ya mawasiliano ya umma na nina uzoefu mkubwa katika eneo hili na nishakuwa sugu na changamoto za kazi."


"Halafu waulizeni Simba namuachia nani ? Alihoji @hajismanara


#Manara amedai kuwa, huenda ukubwa na umaarufu wa jina lake unamponza hadi kufikai hatua ya kuzushiwa mambo kama hayo, lakini anahisi huenda hatua ya kuzushiwa majanga inatokana na kazi yake kuwavutia wengi ndani na nje ya nchi.


"Huu ukubwa wa jina langu unaniponza, umaarufu wangu unawaumiza wengine. "Sikuwahi kutaka kuwa hivi, lakini kazi yangu naamini imewavutia wengi na Mungu akaamua kunipandisha."


Ikumbukwe, #Manara aliwahi kutoa ufafanuzi kwa nini amekua kimya kwa majuma kadhaa, akisema uongozi wa Simba SC ulimpa mapumziko (Likizo) baada ya kufunga ndoa na mke wake Naheeda Abdallah, Desemba 10 mwaka huu 2020.

Muuaji hatari katika historia ya Marekani, Samuel Little afariki Dunia



Samuel Little, mtu aliyetajwa na shirika la kijasusi la FBI kama muuaji mkubwa wa kuvizia katika historia ya Marekani amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

Samuel Little, most prolific serial killer in U.S. history, dies

Little alifariki katika hospitali mjini California siku ya Jumatano, idara ya magereza imesema. Alikuwa akihudumia kifungo cha mauaji ya wanawake watatu

Lakini kabla ya kifo chake , alikuwa amekiri kuwauawa wanawake 93 kati ya mwaka 1970 na 2005.

Little aliwalenga watu waliokuwa hawawezi kujitetea, wengi wao wakiwa makahaba ama watumiaji wa mihadarati , walisema maafisa.

Little alikuwa akiuwa bila kuwacha ishara zozote za mauaji, kama vile kuwadunga kisu ama kuwapiga risasi na kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa.

Badala yake vifo vyake vingi alivyo uwa vilidaiwa kula dawa kupitia kiasi ama vya ajali na havikuchunguzwa. Baadhi ya miili haijapatikana , kitengo hicho kilisema.

Mwaka uliopita FBI lilisema kwamba wachambuzi wake walisema kwamba madai yote aliokiri kutekeleza yalikuwa ya kweli.

Pia walitoa picha za waathiriwa aliowachora wakati akiwa jela katika jaribio la kuwatafuta aliowaua,Waathiriwa wa Samuel Little

Shirika la FBI lilitoa michoro ya Samuel Little kwa matumaini kwamba waathiriwa watatambulika
Little alikamatwa mwaka 2012 kwa mashtaka ya kutumia mihadarati mjini Kentucky na kusafirishwa hadi California, ambapo maafisa walitafuta vinasaba vyake .

Tayari alikuwa na rekodi mbaya ya uhalifu akiwa na mashtaka ya wizi wa mabavu hadi ubakaji katika maeneo mbalimbali Marekani.

Vinasaba vya DNA vilimuhusisha na mauaji ya watu watatu ambao hayajatatuliwa kutoka 1987 na 1989 katika kaunti ya mji wa Los Angels.

Alikataa kufanya makosa lakini hatimaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha , bila fursa ya kuachiliwa katika siku za usoni.

Ramani ya kifo kinachohusishwa na bwana Little kutka kwa data ya FBI
Ramani ya kifo kinachohusishwa na bwana Little kutka kwa data ya FBI
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...