Mabingwa wa Nchi Simba SC imetajwa kama Klabu namba moja duniani ambayo ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Istagram kukua kwa kasi na kuzipiku Tottenham, Sevilla, Inter na timu nyingine.
Takwimu hizo zimetolewa na mtandao wa Transfer Marketing unaojihusisha na maswala ya mchezo wa soka duniani.
Kwa mujibu wa transfermarket, Simba SC imeshika nafasi ya kwanza kwa akaunti yake kukuwa kwa kasi zaidi duniani kwa asilimia +89, ikiwa na wafuasi Mil 1.9 ikifuatiwa na Trasfermerket nafasi ya pili kwa asilimia +76 wafuasi Mil 3.9 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Leverkusen ikiwa imekuwa kwa asilimia +66 huku wafuasi Mil 1.1
Kwa upande wao Simba wameandikwa ujumbe ufuatao "Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market, Simba Sports Club ndio klabu ambayo imeongoza duniani kwa ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Istagram kukua kwa kasi. Chama kubwa hili weka mbali na watoto." – Simba SC
Oktoba 22/ 2020 Mtandao huu uliwahi kumuandika Mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki, Mbwana Samatta kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wametembelewa zaidi kwenye mtandao wa Transfer Marketing wakati wa dirisha la usajili wa majira ya Joto.
Kwa mujibu wa transfermarket, Samatta ametinga tatu (3) bora kwenye Orodha hiyo inayoongozwa na mchawi wa soka Lionel Messi nafasi ya pili ikichukuliwa na fundi wa mpira Cristiano Ronaldo huku ya tatu ikienda kwa Mtanzania, Captein Diego, Samatta.