Samirah Yusuph.
Maswa. Kukamilika kwa ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi wilayani Maswa imetajwa kuwa ni moja ya sababu za kutokomeza magonjwa ya mlipuko wilayani hapo.
Ujenzi uliogharim kiasi cha shilingi milioni 178.7 kukamilisha matundu 125 katika shule saba za msingi itakuwa ni msaada kwa wanafunzi na jamii katika kujilinda na magonjwa hayo kwa matumizi sahihi ya vyoo.
Ambapo mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Fedrick Sagamiko alisema ujenzi umekamilika kwa asilimia 95, mradi uliotekelezwa kupitia programu ya Afya na Elimu shuleni (SWASH) katika awamu ya kwanza, alisema:
"Ni mradi wa benki ya dunia lakini upo chini ya usimamizi wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) mradi huo unatekelezwa katika shule ambazo zilikuwa na changamoto ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na walimu".
Sagamiko Alizitaja shule hizo kuwa ni Jija A matundu (20), Malampaka(33), Mandang'ombe(7), Maswa(30), Mwabulimbu(15), Mwashegeshi(9) na Sangamwalugesha(11).
Katika ujenzi huo kuna mambo ya msingi ambayo yamezingatiwa ambayo ni elimu,afya na maji kwa lengo la kutunza mazingira na kuwa msafi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.
Alisema kuwa wamehakikisha vyoo hivyo vinakuwa na mfumo wa maji ili mtumiaji mara baada ya kutumia ananawa mikono na kuwa msafi na hivyo kujiepusha na aina yoyote ya magonjwa yanayotokana na uchafu na kuongeza kuwa:
"Ujenzi wa vyoo hivyo umechangiwa na wananchi wa maeneo husika huku akiwashukuru kwa kujitoa katika kushiriki na kuhakikisha vyoo hivyo vinakamilika".
Awali Afisa Elimu Msingi wilaya ya Maswa Saimon Bujimu, alihakikisha kuwa kwa ushirikiano na wakala wa maji wilayani hapo wataweza kutatua changamoto ya maji katika shule hizo ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira safi na salama".
MWISHO.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
